|
| |
| |
TOPIC: Dawa ya ukimwi kupatikana
|
|
Wana HY nimeona leo nianzishe haka kamjadala ka dawa ya ukimwi kupatikana kwa sababu binafsi naona kama watu wanapotoshana or zaidi wanaharibiana maisha. jana nilikuwa bar moja hapa jijini mimi na rafiki zangu na pembeni yetu walikuwa wamekaa wanaume kama watano ambao wengi wao walikuwa na pete za ndoa mkononi wakaanza haka kamjadala ka dawa ya ukimwi kupatikana basi wakawa wanasifia sana kwamba sasa hivi mambo mteremko yani kupiga nje kwa sana tena kula pipi bila maganda yani wakaanza kunywa huku wanasherehekea kupatikana kwa dawa huku wakisifia kuwa sasa hivi mambo mteremko watatoka nje kwa saana. Mimi nimejaribu kufuatilia hii habari ya dawa kupatikana na binafsi naona si dawa kabisa kama wengine wanavyosema bali ndio mwanzo wa kutengeneza dawa, kuna gazeti limeandika inatibu asilimia 99 jamani hii ni kweli?? any way sitaki kuamini sana hizi habari au kutoziamini lakini hoja kwetu kweli dawa kupatikana ndio iwe kichocheo cha ngono?? mimi naona inasikitisha sana watanzania wanandoa tunavyokuwa na akili fupi kiasi hiki cha kuchochea ngono kisa dawa ya ukimwi imepatikana kweli hata mumgu hatumuogopi?? |
| |
Topic by: Date: 2010-07-23 |
|
|
| |
|
|
|
| |
E-MAIL ME FOR NEW POST |
|
|
 |
| |
|
|
| |
Mdau shukran kwa kuleta mada hii imenigusa sana maana niliposikia hiyo habari nilifurahi sana km dawa imepatikana iwasadie wagonjwa mateso wanayopata ni makubwa sana. But on the other hand nilifikiria sana mitikisiko kwenye ndoa na familia kwa ujumla sijui kama itavumilika. Lkn bado safari ni ndefu sana hadi dawa iingie sokoni. Tuombe Mungu na tutarajie watu kupotoka zaidi. |
|
| |
Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 01:57:14 [Report Abuse] |
|
|
 |
| |
|
|
| |
Kwanza futa usemi "INASIKITISHA WANANDOA TUNAVYOKUWA NA AKILI FUPI KIASI HIKI CHA KUCHOCHEA NGONO" japo mimi ni mwanandoa lakini sina akili fupi unayoelezea. PILI-------- Dawa ya ukimwi bado haijapatikana. Wapo katika stage 2 ya kupata vaccine au kinga. Hii ni habari nzuri kwa wale ambao hawana maabukizi kwani unaweza kupata Vaccine ya kutokupata maabukizi. Pia ni habari nzuri kwa wale wenye virusi kwani itawazuia kutokupata maabukizi zaidi ya yale waliokuwa nayo. Ni habari njema pia kwani MPAKA HAPO NI HATUA NZURI YA KUELEKEA KUPATA DAWA YA UKIMWI. ILA KUMBUKA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! HAKUNA DAWA HATA MOJA DUNIANI AMBAYO INAWEZA KUUWA VIRUSI vya aina yeyote ile. HAKUNAAAAAAAAAAAAAAAAAAA. MFANO..... MAFUA YA KAWAIDA YANASABISHWA NA VIRUSI NA HAKUNA DAWA MPAKA LEO. DAWA UNAZOTUMIA NI KUSUPRESS VIRUSI LAKINI HAVIFI. KUMBUKA KUWA HII VACCINE AMBAYO IPO STAGE TWO IMETOKANA NA ANTIBODIES ZA MWANAUME SHOGA NCHINI MAREKANI (black american) Kwahivyo wapo watu duniani ambao wameshawahi kufanya na mapenzi na wenye virusi lakini hawajapata maambukizi. Ina maana kinga yao ya mwili ipo juu sana na virusi haviwezi hata kupenya. ila hiyo issue ya wanandoa kushangilia mi hata sielewi. |
|
| |
Reply by: jogoo, Date: 2010-07-23 02:41:37 [Report Abuse] |
|
|
 |
| |
|
|
| |
kumradhi wadau na mdau jogoo keyboard iliteleza tafadhali weka neno baadhi ya wanandoa kabla ya hiyo statement. kukosea kupo tusameheane nilikuwa nareffer hao mabwana walokuwa wanadiscuss na wanashehekea kufanya ngono zembe nje ya ndoa zao kisa dawa imepatikana hao na walio na tabia kama zao ndio wenye akili fupi. |
|
| |
Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 03:08:47 [Report Abuse] |
|
|
 |
| |
|
|
| |
Wana HY hii mada kwa asilimia kubwa itakuwa ya kutunga ndio maana aliyeitoa hakujitambulisha.Nafikiri ifike hatua tuwe makini kidogo maana jamvi hili si la kusambaza umbea au wakati mwingine udaku wa mitaani ambao umetokea kupendwa na kuendekezwa na watanzania wengi sana kwa miaka ya karibuni.Na wakati mwingine inashangaza sana hata wale wenye heshima zao na walio kwenye Ndoa wanayaendekeza haya na kupotosha jamii nzima ambapo matokeo yake tunajionea hivi sasa.Ni kweli "Utandawazi" umetuvuruga sana haswa nchi zetu zinazoendelea lakini inapofikia hatua ya kushabikia udaku haswa kwenye jamvi la watu makini kama hili basi jamii nzima inakuwa imevurugwa kiasi cha kutosha.Hivi unaanza vipi kuwashawishi wana HY makini kuwa wanaume wanandoa watano wanakaa pamoja na kuzungumzia ukware sababu dawa ya kupunguza makali ya Ukimwi kupatikana.Ni kitu ambacho si kweli kwa uhalisia wa nyakati hizi pamoja na kuwa mmomonyoko wa maadili umekuwa kwa kasi ya ajabu ktkt miaka ya karibuni haswa kwa wanandoa wenyewe.Hivyo wana HY tujaribu kuwa makini na wakweli tunapotoa mada zetu na si kupotosha taasisi nzima ya 'Ndoa" ambayo pamoja na wahusika wachache kuivuruga bado ni msingi na agano muhimu kwa maisha ya wanadamu.Cha msingi ni kuendelea kurekebishana humu pindi inapowezekana na si kuongea au kushabikia majungu yasiyotusaidia zaidi ya kutupotosha.Ni mtizamo wangu |
|
| |
Reply by: Mushobozi, Date: 2010-07-23 04:45:01 [Report Abuse] |
|
|
 |
| |
|
|
| |
Kwa kweli mimi sijali kama ni umbea au ni mada, ila napenda kuchangia kidogo mambo ambayo nayasikia huko mtaani nay ale ninayoyajua. Kama jogoo alivyosema, dawa haijapatikana ila kuna maendeleo mazuri katika kutafuta dawa ya ukimwi. Kwa wale waliosoma biolojia kidogo, virusi havifi hasa vikiwa nje ya mwili wa kiumbe hai yoyote. Nilivyosoma makala ya hawa wamarekani, inaonyesha kuwa ni hatua nzuri, mimi ni mwanabiolojia. Hata hivyo, bado kazi ni kubwa ya kufanya ili dawa ipatikane. Ninachokishauri, hata kama kusingekuwa na ukimwi, kufanya uasherati na uzinzi ni dhambi na hata kama isingekuwa dhambi, ni jambo baya sana. Kwa hiyo, hawa wanaojipa moyo kuendelea kufanya uzinzi na uasherati kwa kupatikana kwa dawa, japo sio kweli kwa sababu ni hatua tu katika kuelelea kupata dawa halisi, wanafanya makosa makubwa. Mimi nadhani serekali itoe elimu ya tafsiri ya kile kilichoandikwa. Mkutano wa dunia unaohusu ukimwi unaanza hivi karibuni kwa hiyo wale jamaa walikuwa na nia ya kuuambia ulimwengu walipofikia kama watakavyosema kwenye mkutano wa dunia. Nawasihi watu wote walioko hapa wajue ya kuwa uzinzi na uasherati ni dhambi mbaya sana kwa hiyo hata kama kusingekuwa na ukimwi, mambo hayo hayafai katika jamii. Chanzo cha malalamiko na simanzi kwenye ndoa nyingi yanasababishwa na hayo mambo. Nawatakia weekend njema |
|
| |
Reply by: mbwange, Date: 2010-07-23 05:19:07 [Report Abuse] |
|
|
 |
| |
|
|
| |
MUSHOBOZI NAKUPONGEZA KAMA WEWE HUWEZI SHABIKIA LAKINI PIA NAKUPINGA KWAMBA WANAUME HAWAWEZI KUSHABIKIA WAKIWA WATANO MEZA MOJA, BINASFI NIMEONA KWA MACHO YANGU WATU WAKIONGEA JAPO WANAFANYA KAMA UTANI LAKINI WANAMAANISHA KUFURAHIA KUPATIKANA KWA DAWA KWA MINAJILI YA KUJIRUSHA BILA WASI WASI SASA KAMA WEWE UNAONA HAIFIKIRIKI NI WEWE ILA NADHANI MTOA MADA HAKUWA NA SABABU KUANDIKA TU FROM NO WHERE HATA HIVYO HILI NI SWALA LA MUHIMU SANA NA HAPA HY TUNATAKIWA TUSHAURIANE NA TUKUMBUSHANE HAYA MAMBO MTOA MADA HOYEEEEEEEEEEEE |
|
| |
Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 06:58:09 [Report Abuse] |
|
|
 |
| |
|
|
| |
pia nailaumu serekali yetu kwa kuwa kuna gazeti moja limeandika Tanzania kuwa ya kwanza kupata dawa ya ukimwi, hii inaleta matumaini makubwa ni sawa lakini pia inaharibu maadili kama inavyosemekana si kwamba dawa imepati kana lakini possibility ya kupata vaccine ni kubwa sasa hili swala la communication hapa nchini kwetu litawacost sana watu wanaoamini kila wasikialo kwenye vyombo vya dola na cha kushangaza wizara ya afya haijatoa tamko lolote juu ya hili. |
|
| |
Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 07:04:59 [Report Abuse] |
|
|
 |
| |
|
|
| |
Binadamu ni viumbe wa ajabu kweli. Kwa hiyo hao wakware kusikia dawa ya ukimwi imepatikana basi ndio wanaona mambo safi. Hivi mbona tu hawatumii akili kidogo.. Dawa ya malaria si ipo? lakini mbona malaria ni ugonjwa unaoongoza kwa kuuwa watu katika nchi za joto? Kwa nini tunashauriwa tujikinge na mbu wa malaria wakati dawa ipo??? Jamani, Njia sahihi ni kujiepusha na uasherati/uzinzi na sio kushangilia kwamba dawa imepatikana. Kuzuia ni Bora kuliko tiba. |
|
| |
Reply by: Daniella, Date: 2010-07-23 07:06:39 [Report Abuse] |
|
|
 |
| |
|
|
| |
Eti watu wanasherekea dawa imepatikana..kwa kweli nakubaliana na mtoa mada kwamba hiyo akili ni fupi..no wonder Afrika hata dawa ikipatikana watu wataendelea kufa...L |
|
| |
Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 09:05:33 [Report Abuse] |
|
|
 |
| |
|
|
| |
Na tena kwa afrika yetu, dawa ikipatikana watu wengi zaidi ndio wataambukizwa bec si wanajua kwamba dawa ipo, basi ngono ambazo si salama kwa kasi..mhh how stupid.. |
|
| |
Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 11:20:59 [Report Abuse] |
|
|
 |
| |
|
|
| |
Joggo umesema vyema na umesema hasa kilichopo tofauti na ilivyotangazwa ingawa leo nimemsikia mtu mwingine wa wizara akitoa maelezo..alichosema Jogoo ndicho na sio kwamba kuna dawa..hao washangiliaji huwezi fanya kitu wenye akili upupu wako kila kona |
|
| |
Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-23 20:13:02 [Report Abuse] |
|
|
 |
| |
|
|
| |
Ni kweli kabisa watu wanashangilia kabisa kupatikana kwa dawa mimi binafsi nimeshashuhudia zaidi ya watu kumi hapa kazini kwangu wakifurahia tena kwa kugongeshana mikono na wengine ni wanawake wakisema Aaah shida iko wapi saizi hata nikimkuta anakohoa simuogopi' jamani minadhani kupatikana kwa hizi dawa sijui maana nadhani Mungu anaweza akatuangamiza kama SODOMA NA GOMMORA |
|
| |
Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-27 04:07:58 [Report Abuse] |
|
|
 |
|
|
| <<Back to Topics<< >> Reply to this message>><<EMAIL ME FOR NEW POST << |