Home
About Us
Photo Gallery
Home
Planner
Planner
 
  TOPIC: Ni Robo Tu Ya Wanaume Wa Dar Wenye Mbegu Zenye Rutuba

 

http://learnshareandinspire.blogspot.com/2010/07/ni-robo-tu-ya-wanaume-wa-dar-wenye.html
  Topic by:JJ Date: 2010-07-22   
       
  E-MAIL ME FOR NEW POST    
     
  baada ya kunywa uji wako wa mchele asubuhi, ukaona uheme huku unadonoa kama kuku kwenye laptop ya shangazi/mjomba. UNATOA TU MADA BILA HATA KUFANYA RESEARCH. watu wengine mkijisikia kukuna mikono yenu mnakuja kwenye computer kusugua keyboard. huna data hata moja. kisa tu kuwa wewe huna mbegu zenye rutuba unafikiria ni kila mtu. Ndiyo maana afrika tunawaza kurogana tu. mtu hulali usiku unaruka tu na ungo kwa sababu mwenzio ana maendeleo. UNAJUA KUNA WANAUME WANGAPI TANZANIA???????? UMESHAWAHI KUPIMA WANAUME WOTE TANZANIA UKAPATA JIBU LAKO LA UJI WA MCHELE? MAFENESI YALIYOTUNGULIWA YAKAANGUKA CHOONI!!! MIMI HATA SIELEWI.  
  Reply by: jogoo, Date: 2010-07-22 02:36:58 [Report Abuse]    
     
  Yaani nimeingia hapa nikasoma hii mada nikasema leo humu kama kungekuwa hakuna mchujo wa administrator ingekuwa ngondo kweli, maana umechokoza nyuki za watendewao zitakuuma mpaka. Niliposhusha macho yangu hapo kwa mchangia mada wa kwanza, nilikuwa nakunywa chai yangu wacha inikwame na kuanza kukohoa yaani nimecheka mpaka machozi yamenitoka, asante kunitengenezea siku yangu hahahahahahahah. Jamani mbona tunazalishwa usiku na mchana huku wajemeniiiiiii?  
  Reply by: Salua , Date: 2010-07-22 02:55:57 [Report Abuse]    
     
  Duh! Kaz kwel kwel........!  
  Reply by: Pozi, Date: 2010-07-22 03:04:15 [Report Abuse]    
     
  Mh! Huku kuropokaropoka huku kwingine  
  Reply by: mbwange, Date: 2010-07-22 03:25:19 [Report Abuse]    
     
  Wanaume wakiguswa penyewe wanakuwa wakali kweli!  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-22 03:41:30 [Report Abuse]    
     
  Kwa hiyo tufanyeje? tuseme Ndiyo au Hapana?  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-22 03:43:26 [Report Abuse]    
     
  Jamani jogoo....mi hoi huku , maana tangia asb nilikuwa cjacheka  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-22 04:28:49 [Report Abuse]    
     
  kwi kwi. kwi, teh teh teh, jogoo umegonga ikulu watakushambulia hao  
  Reply by: dada neema, Date: 2010-07-22 08:03:22 [Report Abuse]    
     
  mie yangu macho nimecheka almanurusura nifumwe na boss wangu ingekuw akweli jamani ndo muhimbili mwananyamara temeke na kwingineko kungekuwa busy kwa kufyatua watoto kweli ya leo kali jogoo ukosagi la kusema jamani kweli wewe noma lakini bora na nye wanaume mmepashwa leo mbona mpo kimya tena jibuni mapigo msimwachie jogoo awajibie  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-22 09:45:03 [Report Abuse]    
     
  teh teh teh..at least hata wanazo za kumwaga basi manake nazo ingekua hakuna ndo pangekua patamu..sasa jogoo mbona umekasirika saaana jamani si katoa tu link na kinachosemwa..teh teh uuuuwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii..manake nimecheka ghafla na maji yangu kinywani  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-22 10:05:32 [Report Abuse]    
     
  leo naona kaka zetu wameguswa kasheshe kweli..ila mie naona robo sio wengi so Jogoo usiwe na wasiwasi..na wanaume wa kiafrika wasivyopenda kupima afya zao za uzazi basi hapo kimewaume sanaaaaaaaaaaaaaaaaaa..-PJ  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-22 10:15:58 [Report Abuse]    
     
  Kweli kabisa PJ wanaume zetu huku kupima afya hasa uzazi ni mtihani mkubwa. Yuko radhi akajipimie nyumba ndogo mwisho anadanganywa kwa kubambikiwa lakini kwenda kujicheki na kujitibu hapana anang'anga'na mi mwanamme rijali bwana, urijali na mbegu ni vitu viwili tofauti kabisa. Matokeo yake mzigo ule anaubeba mke kelele kila cona mawifi wakwe majirani mwanamke yule hazai kumbe tatizo liko upande wa pili labda angefanyiwa uchunguzi wa kina wangepata suluhisho.  
  Reply by: Salua, Date: 2010-07-23 00:53:00 [Report Abuse]    
     
  ehh Salua na PJ bora mseme, kuna rafiki yangu mmoja aliolewa kakaa na mumewe for 11 years hakuna mtoto, basi mume sio matusi hayo na kumuita majina, mara amfukuze kwamba hazai, anamjazia choo, kakaa baada ya miaka zaidi ya 12 mume kaamua kumuacha kwa talaka na vishindo..akaondoka zake..si kauguza maumivu baada ya muda kaamua kuanza uhusiano yaani hata uhusiano haujajulikana kwa watu mdada mjamzito..imagine..kumbe si ajabu mume ndo alikua tatizo na sio yeye...Salua umenimaliza na kwamba urijali na mbegu tofauti...manake mwingine akiona inasimama anajua ndo na mbegu bora..teh teh teh kumbe upepo wa msituni...marianyafuru  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 01:56:43 [Report Abuse]    
     
  mmmmmh  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 02:59:55 [Report Abuse]    
     
  Maria......yeuwiiii...sitaki mie!!! ha ha ha ha....upepo...yalaaa!  
  Reply by: Pozi, Date: 2010-07-23 05:59:03 [Report Abuse]    
     
  Hii topic hapa ni mahali pake. Ni vema tuwe tunaambiana tu ukweli wa wanaume wetu wa kiafrika. Mie nipo huku ulaya mdada kaja na mume wameoana huko bongo..mdada akapenda kupata mtoto kajaribu wee wapi. Kwenda hosp ma Dr. wanamwambia mbona hamna tatizo tunaomba uje na partner wako..Duh mkaka si kakataa kabisa kwenda na kujibu mwanaume wa kiafrika hapimwi afya ya uzazi..mke mbembeleza wee baada ya mwaka ndio kukubali kwenda kupimwa tena wote wawili..Mbona ilijulikana mume ana tatizo fulani inabidi afanye minor operation then mambo yatakuwa mazuri..kafanyiwa kajiopereni after 6 months mke mjamzito. Sasa kasheshe ilikuja kwamba mume kumweleza Dr. kwamba mbona yeye huko bongo ana watoto 2,..Dr. akamjibu hiyo hawezekani, ila whatever waletwe hao watoto tupime with a very simple test ect mume kanywea maana yaelekea alikuwa anatunza watoto sio wake ect..kasheshe..-ÖÖ  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 07:14:50 [Report Abuse]    
     
  Da Salua acha kunikichekesha eti ´Yuko radhi akajipimie nyumba ndogo´huko hataambiwa kwamba hazai bali atabambikiziwa mtoto tena kirahisi tu na baada ya hapo anachorwa kwa kusifia watoto jinsi wanavyofanana na yeye jamani kaka zetu ni kazi kweli kweli..Da Maria hiyo ya kuzaa baada ya kufukuzwa kwa mume mbona wengi tu inawatokea..mimi nilishasikia story kama hiyo..mwisho wa siku ndugu za mume wakawa wanamsema huyo dada kwamba eti alikuwa hataki kuzaa na ndugu yao´..ila nadhani wenyewe mwisho wa siku walijiona wanajichanganya wakaamua kukaa kimya...na huyo kaka nilishwa onyeshwaga masikini siku hizi ni kama mlevi fulani hivi naona ndio hizo fustruction...Mama KK  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 08:58:36 [Report Abuse]    
     
  mhh hii dunia kuna vituko jamani sasa jamani wewe OO hiyo story imeishia wapi maana mume wa mtu anatunza watoto na kujigamba huko kumbe sio wake..aisee kuna kazi hapo..-Ke  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 11:17:02 [Report Abuse]    
     
  jamani sina uhakika kama hizo takwimu ni kweli, ila wanaume wengi sana huwa hawapendi kabisa kwenda kuangalia afya za uzazi,mfano mimi nimeoana na mume wangu toka tar14 april 2004,toka hapo tukakaa miaka mi5 bila mtoto.kila nikimwambia tukapime hataki.basi mi nikaenda kwa dr nikapimwa na nikakutwa sina tatizo,nikaja kumwambia mwenzangu kuwa mi nimepima na dr kaomba twende tukaangaliwe wpte kama ni tiba atupatie.mwenzangu akakataa kabisa.tena ndo akatafuta Gf ili ajipimie huko,akakaa na huyo mwanamke wee kwakua huyo mwanamke alishazaa b4 na mwanamke mwingine,akaiba namba zangu kwa simu ya mume wangu akaanza kunitukana na kudai mimi TASA kwakweli iliniuma sana nami nikaamua kuchepuka nje.mungu si athumani nikadaka mimba na sasa nimejifungua mtoto wa kike na hajui kama si wake,kutwa tu kujitapa kwa rafiki zake kuwa eeh uvumilivu hula mbivu kumbe mi namn'gong'a tu kisogo. sasa hapo angetoa ushirikino na kwenda kupima tukajua tatizi wala nisingefanya hili nililofanya!na si mimi tu nauhakika wengi sana wamefanya kama nilivofanya mimi mradi ndowa zao aiwe na amani! maana yule gf alivoonekana hashiki mimba nae alipigwa chini!  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 12:18:59 [Report Abuse]    
     
  We shosty hapo juu balaa, umeamua kubeba mimba nje kwa kumkomoa mumeo maana mbishi kwenda kupima. Mwenyewe anajisifu kujiona kidume cha mbegu kumbe hana lolote. Huyo akikua nenda tena nje katafute mwingine huyo mwanaume muwache na ubwege wake. Halooooo halooooooooooo  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 13:01:23 [Report Abuse]    
     
  Anony uliyebeba mimba nje ya ndoa umefanya la mbolea! Bora ulivyo muwahi huyo mwanaume ukaamua kuzaa nje ili ujipatie mwanao. Alitaka wewe ubakie childless halafu uanze kulia peke yako na upweke wakati yeye anakwenda nje kutafuta mtoto. Wanaume ni wabinafsi sana. Inabidi na wanawake na sie tuwe wabinafsi hivyo hivyo. Ubaya ubayana.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 14:23:41 [Report Abuse]    
     
  I wish wanaume wengi wangekua wanaingia hapa wapate kujifunza yanayojiri maana teh teh teh! sina mbavu kwa jinsi wanavyokula jeuri yao. wanaume wetu wa bongo hawa teh teh teh! Pole zao kwa kulea watoto wa wenzao.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 14:45:54 [Report Abuse]    
     
  Mdada uwe makini lkn usirudie tena akikugundua huyo atakuvunja mbavu teh teh teh!  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 15:03:07 [Report Abuse]    
     
  mh! jamani kwa hilo la kubeba mimba nje ya ndoa naomba tusipongezane akae kwanza kimya maana huwezi jua mie mume wangu alibeba watoto wake akasema anaenda zanzibar kutembea na watoto kumbe kaenda nao nairobi kwa kaka yake kuwapima DNA aliporudi kaja macho kayatoa ananiambia una bahati nimekuta watoto ni wa kwangu maana ungenitambua wanawake wa sikuhizi amuhaminiki nilibaki mdomo wazi na hasira nikamuuliza huniamini wala hakujibu mama uliyechit kaa kimya wanaume wa siku hizi wanalijua hilo ndugu yangu.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 15:13:33 [Report Abuse]    
     
  ehh mate yamenikauka mwenzenu..kwamba wamng'ong'a tu..ehh jamani..Pozi hakuna wine ya baridi jirani?mama KK wewe nisaidie tu nipate nyama choma, jamani serious nahitaji kurudisha mte manake nimekaukiwa...na kweli i wish wanaume wengi wangekua wanakatiza huku ndani..marianyafuru  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 15:15:52 [Report Abuse]    
     
  wala mashost sisubiri akue sana maana mi mwenyewe ni mkubwa sana nishafikisha 35 nasijazaa kawaida,nasubiri tu afikishe miezi 6 nashika nyingine chapchap maana nae nikisema kabaki haka kamoja tu mshkaji atashtukia.cha muhimu ni mtafute huyuhuyu nilozaa nae nizae nae na huyo mwingine ili watoto wawe wa baba mmoja and the good thing huyu mwanaume namjua sana coz alisoma na kakaangu so baadhi ya matatizo najua haya takuwepo kwa watoto wangu,ila kamwe sintakaa nimwambie kama nimezaa nae wala nataka nizae nae maana wabongo nao hawashindwi kukuharibia ati.wanawake wenzangu msilalee jamani nauhakika mi ndo ningekua na matatizo saizi mwenzangu angekuwa watoto huko nje.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 15:18:41 [Report Abuse]    
     
  Uwiii maria namie nipatie ka waine plzzzzzzz huyu dada hapa juu kaniacha hoi mie hahahaahaaa jamani nipeni overmeer (hivi bado ipo?) teh teh  
  Reply by: Daniella, Date: 2010-07-23 15:27:43 [Report Abuse]    
     
  Dada zetu hivi huko kuzaa nje ya ndoa hamuogopi ukimwi? Aisee inatisha sana.-Jim  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 15:45:14 [Report Abuse]    
     
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 15:13:33 huyo mumeo nae sijui akili kaweka wapi..all the trouble za kwenda sijui NBO ect si angejipima tu afya yake kabla ya kupata watoto ect..wanaume wa kiafrika wana tick just different..kasheshe.Na huyo jamani kaenda nje na kuambiwa hawezi kupata watoto mpaka operesheni makubwa kumbe bongo alikuwa anasaidia wenzake kulea watoto international school na kujigamba...mhh kwa kweli hali si nzuri..-MM  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 15:46:40 [Report Abuse]    
     
  Jim usitake watu wakutoe macho! we shauri yako uliza tu maswali ya kimfumo dume mfumo dume!  
  Reply by: No email , Date: 2010-07-23 16:04:13 [Report Abuse]    
     
  @jim,kwani ye alivoenda kutafuta hao watoto huko nje hakujua kama ataleta ukimwi ndani!? kwakweli kosa afanye ,wanamke,akifanya mwanaume kapitiwa na shetani,huyo mume wangu ilifikia kipindi akiwa na huyo msichana anampa apokee simu zangu,na huyo mwanamke alinieleza vitu vingi sana japo ilikua kwa majigambo lakini vyote ni vyakweli,kwakweli nimemkomesha wala sijutii nililofanya.Japo si kwamba naswashauri na wamama wenzangu wafanye nililofanya,lakini kwa mimi acha tu uwe jamani,nimeteseka sana.yaani nikianza kuandika hapa alonitendea.kwakweli ntajaza ukurasa mzima!  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 18:57:00 [Report Abuse]    
     
  Kwa Kweli Daniella mwenzangu mie sina neno kunywa wine yoyote utakayo.. ungekua karibu hapa ningekutafuta kwa kweli tupate moja ya baridi manake huyo dada kaniacha hoi..ehh..human beings jamani watizame tu..sasa Daniella sijui inakuaje manake mie nishaianza weekend.....marianyafuru  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 20:02:02 [Report Abuse]    
     
  wine nitaleta msiwe na wasiwasi cjui maria na kk mwataka ipi (am at your service).....mdada kanichekesha yuko sharp hatki kusubiri hata miezi 6 anataka mimba nyingine....ha ha ha ha.....na siri iwe sirini maanake aliyekupa hiyo mimba akijua anaweza kuharibu picha kabisaaaa....wabongo kwa unnecessary malice ndio wenyewe, saa ingine ni kuharibu tu hata mtoto hatamtunza....wikiendi njema wapendwa...mi leo i feel like putting on my dancing shoes..."pachanga" kwa kwenda mbele...hahahaha  
  Reply by: Pozi, Date: 2010-07-24 06:03:07 [Report Abuse]    
     
  Dah HV KWELI WANAWAKE TENA MLIOOLEWA MNA-SUPPORT HUU UCHAFU ALIOFANYA huyu dada?..mdada madhara ya vitendo vyako ni ya kizazi na vizazi..wewe umefikiria simple solution bt hukuona future impact....tena UJUE KUNA MAISHA BAADA YA HAYA YA HAPA DUNIANI AMBAYO NI YA MILELE...UTAMWELEZA NINI MUNGU WAKO?..hv hata amani ya moyoni unayo unapokaa na huyo mume ukiwa na huyo mtoto uliombambikia?.basi kuwa hata na utu umweleze kuwa sio wa kwake?.mbona WANAUME hata tukizaa nje mwisho tunaeleza ukweli?..huu ni ukatili mbaya sana.!!.nilipokuwa mdogo nilikuwa naambiwa baadhi ya WANAWAKE NI WAKATILI SANA kwa kweli sasa naanza KUAMINI..  
  Reply by: sam1, Date: 2010-07-24 12:39:16 [Report Abuse]    
     
  Sam1 hebu tambaa zako huko.. Kunya anye bata tu akinya kuku kaharisha. Eti madhara ya vitendo alivyovitenda huyo dada.. mshxxx@@@???  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-24 13:05:02 [Report Abuse]    
     
  Pozii jamani sasa sijui iankuaje hapa kwa vile ngumu kupata kila kitu hebu tafuta white wine tuuu yatosha kwa leo manake kuna wakati tunahitaji kulift our spirits hasa unapokumbana na madongo makubwa huku ndani..wababe wangu huku ndani walisoma nadhani hii mada na issue ya huyo dada basi nimerudi jioni nasikia tu ehh wanwake bwana, wanawake wabaya saana, wanawake wauwaji..mie kimya mwisho niko kwani wamefanyaje eti angalia huko HY kwenu huko kuna mtu anazaa nje nikasema bwana wee ndo mjue kwamba mnapofanya vurugu kuna wanawake wako equal to the task ahead so think kabla hujaanza vurugu..nikaona nisiendelee saana kufungua mdomo nitafute kizibo ndo akha gals yangu ya wine iko wapi nikajizibilia mbali..."just for clarification..personally sisherehekei cheating iwe kwa mke au mume..ila pia kama binadamu tujue unapomfanyia mtu visa kila mmoja ana namna yake ya kudeal na usaliti na maumivu..unapomruhusu mwanamke wa nje ampigie mkeo simu jiandae kwa kubwa zaidi...anyways ngoja nikae mkao mwema manake Pozi anaaandaa kinywaji huko..weekend njema wadau woote..mdada wa watoto jiandae pia kwa lolote linalokuja mbeleni manake hakuna siri ya milele  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-24 14:22:35 [Report Abuse]    
     
  Sam hakuna anaeshabikia uovu isipokuwa ubaya watu hufunzwa na matokeo yake huwa mabaya zaidi. Hivi we ulishashuhudia wanawake wasio zaa wanavyonyanyasika? Imagine unanyanyaswa na kosa si lako na mwenye tatizo hataki kutoa ushirikiano. Kwakweli mateso wanayopata ni makubwa kuliko kulaumu ni afadhali nyinyi wanaume mbadilike muache ubabe na mtoe ushikiano pale mnapohitajika kufanya vile. Kwanini wanawake wawe victims wa matatizo yenu unnecessarily? Na nani aliwaambia ndoa ni watoto? wote tunajua watoto ni zawadi wasipotokea twamshukuru Mungu na kuangalia jinsi ya kuendelea na maisha lkn wanaume wetu wa kibongo hamkubaliani na hilo. Msipobadilika mtalea sana wa wenzenu maana mtu unavumilia hadi uvumilivu unafika mwisho. Mdada be careful mi nadhani maadam Mungu kakujalia huyo mmoja ungeishia hapo yatosha kukusafishia nyota siku likisanuka hali itakuwa mbaya na km alivyosema Maria hakuna siri ya milele.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-24 17:19:30 [Report Abuse]    
     
  Dada hebu ongeza tu hata huyo wa pili. Kama ni kosa umeshafanya. Kwani unafikiri akigundua huyo mmoja patakalika? We ongeza wapili na wa tatu kabisa. Akigundua juu yake bora wewe una watoto wako. Wewe sio wa kwanza. Raha jipe mwenyewe bibi....  
  Reply by: No email , Date: 2010-07-25 04:15:36 [Report Abuse]    
     
  @Sam1. Kaka yetu hamna mtu anayesherekea tabia mbaya humu ndani. Na wengi wetu tumeolewa na kasheshe wanazopata wasikuwa na watoto tunaziona tena kila siku. Of course ni result ya mfumo dume kwa afrika. Maana huku ulaya mbona tunaona wadada wengi hawajaliwa watoto na wala wanaume zao hawafanyie vituko, na wanaishi maisha ya ndoa tena kwa raha zao na ku accept kwamba mungu awajawalia watoto. Wanaume kutoka nje ya ndoa na kutafuta watoto huko (as much as wazungu tunawachikia kwa mambo mengi ila kuna vitu lazima mwanaume wa kiafrika ajifunze ktk kwao). Maana hapa mimi ninapoishi kuna mdada mwafrika hajabarikiwa watoto, wala mume hajamletea vituko, na most of the time anasema hapa ningekuwa nimeolewa na mbongo mbona ningekoma ect. So kaka zetu, nyie ndio muwe mstari wa mbele kutoa ´ushirikiano´kwa wake zenu, in the sense kwamba muende wote kupima afya za uzazi na kutafuta solution PAMOJA sio wewe kama mwanaume unadhani eti solution ni kutafuta mwanamke mwingine. Wanaume wengi wa kibongo wanadanganywa sana maana leo hii wewe uende nyumba ndogo na kutoa siri za mkeo kwamba hazai, hivi wewe kwa akili yako unadhani hiyo nyumba ndogo itakuambia kwamba hauwezi zaa? Maana atajaribu miezi kadhaa akiona mambo yako hayaeleweki anajitosa kwa mwingine na kukuletea mimba ambayo si yako. Na hapo wanaume ndio anajiona kumbe mie nazaa kumbe wapi ect. Maana jamii ya kiafrika mume akizaa nje anaonekana bora sana ila mke nae akifanya hivyo ni balaa. Na vile vile ktk topic za mume kuzaa nje mbona hasemi kwamba mbele ya mungu na yeye atasemaje? Mara nyingi watu wanakimbilia kusema kwamba mke amsamee tu. Mbona ktk hii issue hapa hamna mkaka yoyote anayesema mume amsamehe mke wake kwa kuzaa nje? So SAM we need to change, no you men lazima mchange tena haraka sana. Maana unafika wakati nae mke ni binaadam na anachoka kuvumilia kama MARIA alivyosema.-Ke  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-25 04:19:44 [Report Abuse]    
     
  @sam1 ntamjibu vizuri kesho nikiwa hapa ofisini maana hii comp ya home siiamini sana.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-25 07:59:39 [Report Abuse]    
     
  Dada zetu lakini traditionally wanawake wa kiafrika ni wavumilivu na sio hii style nyie mnayoleta hapa ndani..duh mtu unatoka na kwenda kulala na mtu mwingine unaleta watoto ndani aisee mumeo akijua atakuacha vibaya sana, na sijui utasemaje.. -Deo  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-25 13:51:52 [Report Abuse]    
     
  Lakini kaka zetu mie wala siwaonei huruma..wewe mtu anakueleza vizuri tu twende basi tukacheck kama kuna tatizo wewe unakataa ni haki kweli..au huyo hapo juu eti mwaka mzima anambembeleza mume kwenda kupima afya ya uzazi..mbona ni kichekesho?? Na hapo akiwa anakunywa bia BAR anajiona mwanaume kweli..bwana weee wanaume ni wale wanaonenda na wake zao kupima na kutafuta solution pamoja..ndio maana hao wanaletewa watoto sio wao kulea wala sijawaonea huruma hayo yote waliyataka wenyewe...cha msingi wanaume wa kibongo mbadilike sasa tumechoka kusikia story sijui za kumnyanyasa mke bec hawezi kupata watoto (kumbe asilimia kubwa ni nyie wenyewe ndio hamuwezi kukamilisha mambo) ect..-Mdada  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-25 13:59:58 [Report Abuse]    
     
  Reply by: No email , Date: 2010-07-25 04:15:3 dada acha kuchekesha watu..eti aongeze tu wa pili na watatu jamani dunia ina mambo hii..-Mdada  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-25 14:00:24 [Report Abuse]    
     
  uuuuuuwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii mwaniua mbavu zangu mieeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.....haya weee..  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-25 15:05:06 [Report Abuse]    
     
  Kk Deo dunia inabadilika sasa km nyie kina kk mtaendelea kushikilia ya mwaka arobaini na saba mtabaki hivyo hivyo. Kesi ya hivyo hata mkienda kanisani hiyo ndoa inatenguliwa especially km ulijua na ukachuna usimwambie mwenzio. Kuna kesi nyingi nimesikia kwa wanaume ambao wako honest baadhi wakijua matatizo yao huwaomba wake zao watafute japo mmoja kuondoa aibu ingawa km ingekuwa mimi nisingekubali kwenda huko nje bora tubaki hivyo tulivyo kwakuwa ndoa si watoto.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-25 16:39:18 [Report Abuse]    
     
  Soi dunia imebadilika bali Imekwisha jamani, watu hata hatumuogopi mungu, watu wanakuwa kama wapagani, haya mi hapa sina usemi.  
  Reply by: Salua, Date: 2010-07-26 02:51:56 [Report Abuse]    
     
  Kunyanyasa wanawake ambao wanashindwa kupata watoto ni unyama tu. Mtu anayefanya hivyo hata hamfahamu Mungu. Pia kwenda nje ya ndoa eti kutafuta mototo kwa sababu zozote zile ni uovu tu. Kama kati yenu kuna mwenye matatizo ya uzazi, ni suala la kukaa chini na kupeana support na kupeana faraja ya hali ya juu. In fact, ukimwona mwenzako hana uwezo wa kupata mototo unatakiwa umwonyeshe upendo zaidi ya ambavyo ungeonyesha kama hali ilikuwa njema kwenu. Kuna watu wana watoto lakini si riziki hata kidogo. Najua mzee mmoja hapa ana watoto watano, lakini ninavyoongea leo watoto wakiume ni wala bangi wakike ni machangudoa. Nadhani ni motto mmoja tu ndiye ambaye watu hawajui kuwa yuko salama, nina maana hana ukimwi au ana ukimwi tayari. Kwa hiyo kupata watoto au kukosa si suluhisho la kukupatia furaha katika maisha yako. Najua, mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu na hivyo angependa kushiriki katika uumbaji kwa njia ya kuumba mtu (Kuzaa), na hivyo kukosa hiyo nafasi ya kushirikiana na Mungu katika uumbaji inatia simanzi sana. Na hivyo, mtu ambaye nafasi ya kushiriki katika uumbaji hakupewa, anahitaji kupewa upendo wa hali ya juu. Ni kweli, nimeona wanawake wanaonyanyaswa katika ndoa hata na mashemeji na mawifi zake kwa kukosa uwezo wa kupata mtoto. Huo nauita unyama tu. Hata kwenye biblia ukisoma utakuta Leah akimnyanyasa Raheli kwa sababu ya kukosa watoto kwa Raheli, ule ulikuwa unyama tu. Nadhani mnaikumbuka laana aliyoipata Leah! Kama Leah hakuomba msamaha atadhibiwa kwa dhambi ile tu.  
  Reply by: mbwange, Date: 2010-07-26 03:29:37 [Report Abuse]    
     
  mbwange, unajua tatizo letu waafrika ukifika ktk maswala haya wala hamna anayekumbuka dini..hapo culture ya kunyanyasa wanawake ina take place. Na trust us yaani hii culture ipo imejaa tele ktk jamii ya kitanzania. Mara nyingi mke ndio anaambiwa avumilie ila mume anaambiwa aende kwa mwanamke mwingine akazae huko. Na kama wadau walivyosema mara nyingi huyu mume anaenda kudanganywa huko na huko happy tu. Maana mwanaume wa kiafrika afadhali adanganywe kuliko aende hospitali kupima afya yake ya uzazi..very strange attitude..-PP  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-26 03:30:35 [Report Abuse]    
     
  Indeed when it comes to kukosa mtoto culture yetu haimkumbuki Mungu kabisa. wanachowaza ni kumkandamiza mwanamke bila hata kujua tatizo liko wapi. ndugu na marafiki huwa wanaleta pressure inayopelekea wanandoa kufanya vitendo wasivyotarajiwa kama vile kutoka nje ya ndoa kufanya "test". hii inaleta mtafuruku kwenye ndoa na kuondoa value ya partner mwenzio bila kufikira mlitokea wapi mpaka mkawa pamoja. mi nadhani ukipata mtoto ni kumshukuru Mungu na ukimkosa basi pia utoe shukurani kwani yote ni mapenzi yake. kama alivyosema Mbwange unaweza kumpata mtoto ikawa ni presha ingine kwani sio rizki. mimi nina dada kwenye ukoo presha ilimfanya akaasili watoto wawili msichana na mvulana na pia akamlea mtoto wa kiume wa mumewe. dada alikuwa mfanyi biashara kwa hiyo alijitahidi sana ktk kuwalea na kuwasomesha hao watoto. mumewe alikuwa wala hawajali kwani alikuwa na mke mdogo mpaka umauti ulipomfika. sasa hivi dada mtu mzima na mgonjwa mgonjwa lakini alihakikisha kuwa wote watatu kawapa biashara za ku-manage. wale wavulana wametapanya mali zote na sasa ni walevi wakutupa na kila siku lazima wamfanyie fujo na kumuuliza atakufa lini ili waweze kurithi mali zilizobaki. huyo "binti" yeye kaolewa hana time na mama yake yuko na familia yake hata siku moja ilibidi sisi tumpeleke dada hospitali kwavile binti alisema asingeweza kuja yuko bize kwenye biashara zake.sisi tulipata taarifa kutoka kwa wake za wale watoto wakiume walioambiwa wakifanya lolote ndio siku ya kuachwa. but mmoja had the courage to call us. sasa hivi kila ukiwa na dada anajuta kuwalea hao watoto aliokuwa ana-expect makubwa kutoka kwao. so sometimes we just have to accept what God has given us because he has a purpose in everything He does.  
  Reply by: Pozi, Date: 2010-07-26 04:53:38 [Report Abuse]    
     
  Pozi jamani hiyo story ya ndungu yako is so sad.. Unajua sisi waafrika tunadhani kwamba watoto ndio ukiwa mzee watakusaidia kwa siku hizi sio kila mtoto anafanya hivyo na wengi wala hawaogopi laana ect. Wengine wapo nje ya nchi na wazazi wao hawawatumii hata senti moja..so life imebadilika sana too sad..mungu pekee ndio atamlipa huyo ndugu yenu..-PP  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-26 05:24:49 [Report Abuse]    
     
  Pozi well said.-Ke  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-26 05:33:05 [Report Abuse]    
     
  PP umesema ukweli kabisa. Mimi nilijua kuwa naongea na watu wenye dini, sikujua kuwa wengine wanaziweka pembeni mambo yakiwa magumu. Lakini hiyo inatokana na ubinafsi tu. Watu wanataka kutukuzwa na hawako tayari kumpatia sifa mtu mwingine. Ninachokijua ni kuwa watu wanapooana wanafanya hivyo kwa sababu ya upendo. Nitashangaa sana mwanamke aliyeolewa na mwanaume ambaye mpaka anafunga naye ndoa, huyo mwanaume hajamuambia kuwa anampenda. Mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, anaweza akaamua asikupatie au akaamua akupatie. Kwa kiasi kikubwa mfumo dume unaendekezwa na wanawake, wanapenda kutawaliwa na sisi wanaume tunapopewa nafasi hiyo, tunaifurahia. Nimeona watu wengi siku hizi wanafunga ndoa baada ya kuwapa ujauzito wachumba zao. Sasa nashindwa kuelewa kuwa je, hawa wanapendana au uwezo wa kuzaa ndio umewaweka pamoja? Sasa sijui kwanini mtu aweze kupima ukimwi lakini kupima fertility, uwezo wa kuzaa ashindwe.  
  Reply by: mbwange, Date: 2010-07-26 05:49:08 [Report Abuse]    
     
  Ahsante sana pozi na PP. Hicho nacho ndicho kinawafanya watu waoe. Wakikosa wanaamua kurithi wakijua kuwa watakapozeeka watapata malezi kutoka kwa watoto. Hii nayo ni imani potofu sana. Ninachoamini siku hizi ni kuwa kila mtu ana maisha yake. Japo binadamu tumeumbwa kama social animals, mara nyingi kila mtu anasimama peke yake. Kuna wazee wengi hawapati msaada kutoka kwa watoto wao kabisa na wengine watoto wao wanawasababishia matatizo makubwa tu katika maisha. Kuna wazazi wengine wasipopatiwa misaada ya kifedha na watoto wao wako tayari kutoa laana kwa watoto wao. Nadhani kuna haja ya kubadilisha mtazamo. unapompatia mwanao malezi pamoja na elimu ili ukiwa mzee akulee, umemfanya mtoto kama kitega uchumi tu. Nadhani ndio maana yake, ni kama tu mahali fulani tulienda kutoa mahari, mtu mmoja akatuambia kuwa mahari ya huyo dada yatakuwa makubwa si chini ya milioni mbili kwa sababu dada mwenyewe amesoma sana yule, baba yake amemgharimikia sana kumsomesha. Sasa suala la ndugu kumshinikiza kijana wao atafute mwanaume mwingine huenda ni kwa sababu wanajua kuwa kijana atakosa wa kumlea kijana wao atakapokuwa mzee.  
  Reply by: mbwange, Date: 2010-07-26 06:03:23 [Report Abuse]    
     
  heeeee hii story sikua nimeiona mweeee,,,hahahahahaaaaa jamani wanaume tupime afya ya uzazi sio uchawi na kujaribu nje,mwishowe ndo ivo mwaishia kulea mimba si zenu... wajinga ndio waliwao!!wake uo men n go for test khaaaaa,AZA  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-26 06:49:12 [Report Abuse]    
     
  hiyo ya msaada wa kifedha kaka mbwange kali hiyo..wakati wazazi wanaona wanawekeza kwa watoto wao..teh teh jamani Salute kwa watu ninyi  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-27 01:32:32 [Report Abuse]    
     
  JAMANI MNANIVUNJA MBAVU ZANGU HUKU KWELI HII MADA IMEWAGUSA KINA KAKA  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-27 04:04:58 [Report Abuse]    
     
  Yaani mwenzenu nimechoka ni kwamba wanaume ´Dr. wao ni nyumba ndogo..maana anakataa kwenda kwa Dr. eti anaenda nyumba ndogo kuzaa huko jamani..kwa kweli kaka zetu eti times tunashindwa kuelewa hiyo reasoning wanapata wapi..kama wadau walivyosema hapo juu KAKA ZETU HUKO NYUMBA NDOGO HATA KAMA una tatizo hautakuambiwa bali unabambikiziwa mtoto ambae sio wako.. Sasa kipi bora kwenda Hospitali na kujia kulikoni au kumbambikiziwa watoto au mbao sio wako?..YEAR  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-27 10:36:44 [Report Abuse]    
     
  Kuwasaidia wazazi ni muhimu hasa ktk uzee wao, maana wengine wamesota kweli kutufikisha tulipo asiekumbuka kuwasaidia wazazi anajikosesha baraka ktk maisha yake hasa kwa hali ya kwetu ilivyo. Tofauti na wenzetu flow of wealth commences from the parents to the children but in our case it is from the children to the parents. Itatuchukua muda kubadilika na hiyo ya mtoto kutumika km kitega uchumi haijaanza leo waliosoma mambo ya population wanaelewa. Labda kwa wazazi wachache wenye elimu na uwezo wanaweza kuanza kuwa na mtazamo tofauti lkn kwa wale wa vijijini labda karne kadhaa. Wazazi wengine wamepiga jembe jamani na kina mama hata nguo hawana wanafunga mikwega yao na pini na kula ugali kwa chumvi mradi kuhakikisha watoto walau wanaenda shule leo hii ukifanikiwa ukawasahau hata wasipokulaani laana itakuandama tu popote.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-27 17:12:37 [Report Abuse]    
     
  naona ikulu imegogwa na kiongizi ni bushhhhhhhh yani hapo kichapo tu shost zangu, hawajua kutofautisha mbegu na urijal haooooooooo  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-27 22:33:26 [Report Abuse]    
     
  duuh kweli tujifunze jamani kupitia izi news,,,wabongo tuwe na tabia ya kuzijua afya zetu sio adi mahututi unakimbizwa ICU na daktari akuandikie kula matunda na mboga,,,tuende tukiwa tuna afya tu tujijue kwa lolote  
  Reply by: aza, Date: 2010-07-28 06:11:24 [Report Abuse]    
     
  AZA ha ha kweli wabongo kwenda hospitali ni issue kubwa..hapa tupo ugaibuni na Mr. anatakiwa kwenda check up naona anajizungusha..huku tulipo sisi kuna check ambazo ni lazima kwa mwaka eg. Dental issues ect sasa usipoenda na baadae ukiumwa jino insurance inagoma kulipa, simple because haukwenda for check up. On the other hand mimi nakubaliana na insurance maana it is cheaper to treat ugonjwa ukiwa ktk stage ya mwanzo kuliko ukiwa ktk advanced stage..hemu ngoja huyo mbabe nimuhize aende huko kwa Dentist kesho..-KE  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-28 11:11:55 [Report Abuse]    
     
  Ke itabidi sijui umwage maji ndani na kitandani asiwe na pa kukanyaga, jamani hawa watu..they never grow wala kujitake take..eti hata appointment wewe ndo upige kelele..si ndo maana wajikuta mashavu yanaongezeka unadhani afya kumbe kukurupushana na mtu mzima  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-28 12:21:11 [Report Abuse]    
     
  nimecheka eti amwage maji kitandani kasheshe jamani  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-29 02:04:30 [Report Abuse]    
     
  Maria jamani.....hahahaha...eti mashavu yamefura......and my dia yakifura continously yanachukua sura ya uso wako, basi siku hiyo ukatokea ukatabasamu watu wanadhani unataka kulia...uso umefubaa ka dekio!!!!haukubali pozi lolote!  
  Reply by: Pozi, Date: 2010-07-29 02:18:36 [Report Abuse]    
     
  Ke ni kweli kabisa,naona na bongo ebu waazne tu uyo utaratibu wa check-up iwe ni policy na kila mtu awe na BIMA,ingawa BIMA za kwetu apa zinacover si kila kitu na ni kwa wafanyakazi sanasana,sema na tatizo lingine foleni hosp na vimbwanga vya wauguzi/daktari km huna moyo hosp huingii ndo ivo adi uwe mahtuti haha...ni kweli wanaume wagumu kwenda hosp adi mtu unashangaa jamani kwa dhambi ipi asa hutaki???asa suala la uzazi...me nna desturi ya kujichek angalau jamani kdg  
  Reply by: aza, Date: 2010-07-29 07:34:44 [Report Abuse]    
     
  60% ya wanaume waliopimwa DNA wamegundua kua wanalea watoto wasiokua wakwao. niliposoma hii article about a month ago, nilijiuliza maswali mengi sikupata jibu. asante mleta mada, maana nimejua sababu. bei ya kupima DNA imepandishwa na lazima uwe na kibali kutoka Social welfare na serikali za mitaa ili kutoa sababu maana ndoa nyingi zimevunjika. hiyo ndio bongo, kazi kweli kweli. Poleni kina baba. Msijali lakini, kitanda hakizai haramu.  
  Reply by: Derby, Date: 2010-07-29 08:39:02 [Report Abuse]    
     
  usicheke mwenzangu Ke hawa watu unaweza kuwa na mashavu watu wakdhani kama sio afya basi safura kumbe mwenzangu una mtu mzima ndani..kha..teh teh jamani dekio linavyojua kufubaa na wewe hasa likishakamuliwa ikawa kama linataka kukauka ...teh teh mna visa nyie  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-30 01:49:59 [Report Abuse]    
Submit your comment here...!
  Topic Ni Robo Tu Ya Wanaume Wa Dar Wenye Mbegu Zenye Rutuba
  Reply
  Email Login/Register to use your username! (Click here)
   
  Enter Code
   
     
<<Back to Topics<< >> Reply to this message>><<EMAIL ME FOR NEW POST <<
womens pants, wedding dresses, wedding pictures, women shoes, wedding accessories, women nails, women hair, women message women send off, good wedding shoes and hotels
Any use of materials or photographs from HarusiYangu is strictly prohibited
© 2007. All Rights Reserved Designed and maintained by Bomba Designs