Home
About Us
Photo Gallery
Home
Planner
Planner
 
  TOPIC: IT'S MY STORY

 

Mimi ni mama wa watoto 3,umri wangu 42.Nimeolewa na niko kwenye ndoa yangu mwaka wa 13, na nina kazi yangu nzuri sana tu. Mimi na mume wangu kwa sasa hatuko kwenye wakati mzuri tunalala chumba kimoja lakini kila mtu na kitanda chake huu mwaka wa 3,Na sababu ya kuwa hivyo ni baada ya kumfumania na ugomvi mkubwa tu,Nimeshamfumania mara 2 na wanawake tofauti kesi zetu mpaka kwa wazee zimefika kwa hasira niliondoka. Na nilikaa kwa wazee wangu kwa muda wa miezi 6, watoto ndiyo walionirudisha kwani walikuwa hawali chakula wala kulala wanamtaka baba yao, na wazazi wangu wakanishauri nirudi nyumbani kwangu kwa ajiri ya watoto baba yao aligoma kufika kwetu kuja waona watoto wake( nafikiri labda kwa aibu ya matendo yake),walikonda mpaka hata mimi mama yao nilikonda kwa mawazo ya watoto wangu. japo baba mwenyewe kutoka asubuhi sana akirudi watoto anawakuta wamelala, mara moja moja sana kuwakuta wakiwa macho,hata wakati mwingine fee ya watoto shule nalipa mwenyewe.kwani hapo mwanzo nilikuwa nikimkumbushia alikuwa anajibu majibu machafu na kusema"kwani wewe mama yao unafanya nini". Niliporudi alikuwa anataka unyumba,na mimi nikamueleza kuwa kama anataka turudi kama zamani kwanza ajirekebishe tabia yake na pia akubali kwenda kupima kwani mimi nilienda kupima mara 3 kwa kila baada ya miezi miwili, lakini mwenzangu nilipomwambia kwenda kupima hataki yote hayo hakuweza kufanya hivyo na mimi kwa sasa wala simuulizi kwa lolote hata kama akirudi asubuhi wala simsumbui kwa maswali kwani naamini niko kwa ajiri ya watoto wangu. tunaishi tu kwa ajiri ya watoto lakini mapenzi ya mke na mume hayapo kabisa yameondoka ni kama dada na kaka.Nimeshajitahidi sana kujishusha kwake ili mradi tu arudishe mapenzi kwangu lakini mwenzangu wala hashituki kutwa yuko busy. Hata watoto wake anawasahau,hizo simu za kupigiwa na watu juu ya tabia zake nimezichoka.hao marafiki zake wameacha kuja nyumbani kwani wanasema wanaona aibu kwa anayoyafanya rafiki yao. Sasa basi kuna baba nimefahamiana naye kutokana na kunikuta wakati mwingi nikiwa na watoto wangu kuwapeleka kuogelea naye pia akiwa na watoto wake tumezoeana kwa muda kama mwaka sasa,(hatujafanya kitu chochote kibaya ni marafiki tu) na yeye amenipa story yake kuwa aliporudi kutoka kusoma nje alimkuta mkewe ana mimba ya miezi 5,na kwa sasa hawako katika wakati mzuri, anapenda kuwa na mimi karibu zaidi (yaani kimapenzi), kwa kweli nashindwa kuelewa nimkubali au??..!!.. maana kusema kweli upweke pia ninao. Samahani kwa kuwachosha story ni ndefu.
  Topic by:Poleta Date: 2010-07-20   
       
  E-MAIL ME FOR NEW POST    
     
  Walewale wa kuplay victims. Jaji mzuri hatoi hukumu kwa kusikiliza ushahidi wa upande 1 hata kama unaonekana ni kweli tupu. Nikiichambua riwaya yako, kwenye fani umeweza kweli kuivuta hadhira ila maudhui ndo shaka ilipo. Japo umelisema mwishoni maudhui makuu ni kutaka ridhaa ya dhamira kuhalalisha uhusiano mpya unaotaka kuanzisha na mwogeleaji na mpweke mwenzio. Kwa maelezo yako mwenyewe unakazi NZURI SANA TU so what? Ili 2kuambie umwache mumeo ujitegemee? Je kama hauna kazi nzuri je? Kujishusha c maneno ni vitendo na sitaki niamini marafiki hawataki kuja sababu ya aibu ila yawezekana haupendi wageni. Mi hainiingii akilini hapo pa marafiki. Kifupi ur stori sucks  
  Reply by: Poirot@yahoo.com, Date: 2010-07-20 15:01:21 [Report Abuse]    
     
  Walewale wa kuplay victims. Jaji mzuri hatoi hukumu kwa kusikiliza ushahidi wa upande 1 hata kama unaonekana ni kweli tupu. Nikiichambua riwaya yako, kwenye fani umeweza kweli kuivuta hadhira ila maudhui ndo shaka ilipo. Japo umelisema mwishoni maudhui makuu ni kutaka ridhaa ya dhamira kuhalalisha uhusiano mpya unaotaka kuanzisha na mwogeleaji na mpweke mwenzio. Kwa maelezo yako mwenyewe unakazi NZURI SANA TU so what? Ili 2kuambie umwache mumeo ujitegemee? Je kama hauna kazi nzuri je? Kujishusha c maneno ni vitendo na sitaki niamini marafiki hawataki kuja sababu ya aibu ila yawezekana haupendi wageni. Mi hainiingii akilini hapo pa marafiki. Kifupi ur stori sucks  
  Reply by: poirot, Date: 2010-07-20 15:02:42 [Report Abuse]    
     
  Naona mtoa mada hapo ju hujanipata mimi sitaki ushauri wa kuachana na mume wangu.na kama kuachana ningeachana naye, ila kuwa na mtu yaani kimapenzi ndicho kinachonitatiza. na kuhusu kuja wageni kwangu si kweli eti sipendi wageni. wakija baba hayupo na wala akiwepo hana muda na wageni wake.kwa kifupi nyumbani hatulii.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-20 15:37:18 [Report Abuse]    
     
  Kuanzisha mahusiano ukiwa bado kwenye ndoa si busara hata kdg, utakuwa umejiongezea complications. Km kweli una huruma na wanao mi nadhani ungetulia ufanye kazi uwatunze wanao kuliko kujitafutia matatizo mengine. Hivi maisha bila wanaume hayawezekani jamani?  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-20 16:13:55 [Report Abuse]    
     
  nadhani you need to decide..story ya kwamba unakaa na mwanaume kwa ajili ya watoto mama imepitwa na wakati..how old are your kids?what about you and your life?come on life doesnt stop kwa sababu umezaaa..hebu waondoe watoto kwenye kurudi kwako na deal with the issue.kama unataka kuanzisha uhusiano then you need to leave the husband as well..it doesnt make sense kukaa wakati hamkai..na uliporudi alisemaje, karibu mke wangu,. lets talk au?come on nadhani hebu fungua kwanza vitanzi in your life na kati ya hivyo ni kuamua juu ya uhusiano wako na mumeo..kama ni watoto si watakuja weekend au akiwepo wamuone baba yao then warudi??ushasema hata kuwaona tabu manake anarudi wamelala so what is the use of being there?unless otherwise wataka kuwepo ila wasingizia watoto au hujaamua kuondoka..so kabla ya kuanza chochote na yeyote sort your self out kwanza..na huyo baba sijui na habari yake huko kwake naye needs to sort himself out..ukiamua kuosnga mbele songa mbele na sio kubaki na issues... wewe ni mama lakini una maisha yako pia..wakikua wataelewa..kukaa kwenye mazingira ya baba kurudi asubuhi na kutowajali inawaumiza watoto zaidi ya kujidai kuendelea kuwepo..hebu stand on your feet furst and make sound decisions...usitafute visingizio...ni hayo tu..manake kuzaa na kuwa mama haimaanishi our life stops..no yanaendelea, watoto wana nafasi yao, na una jukumu la kuwafanya wawe happy lakini na wewe you deserve to be happy...na unaposema watoto walikonda na wewe ukakonda..wewe kilichikukondesha nini...vituko vya baba yao, umbali, kutokuja kuwaona watoto au? na ya marafiki kutokuja achana nayo kwanza you have a lot to deal with kwa sasa na hiyo ni kuamua hatima ya maisha yako..all the best..marianyafuru  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-20 18:09:23 [Report Abuse]    
     
  jamani ebu nisaidieni definition nzuri yakuachana, kwani kama mmeshaacha kushiriki tendo la ndoa na mnaishi kama kaka na dada kwenye mambo mengine pia (kutokana na maelezo yako), hamuwezi kukaa mkapanga maisha yenu pamoja wala kulea watoto wenu kwa umoja kama baba na mama, kila mtu anaingilia huku anatokea kule mi sioni kama kuna ndoa hapo kwa mtazamo wangu tayari mshaachana labda ni hilo paa la nyumba ndio linaficha ukweli kuonekana kuwa ni mke na mume. Maisha ni yako na wewe ndio unayajua vizuri kaa chambua mazuri na mabaya ya maisha unayoishi sasa na hayo unayofikiria kuyaendea ya huyo mwingine mliyekutana kuogelea then make dission sidhani kama ntakua sahihi zaidi kama nitakwambia kuwa ujiingize kwenye uhusiano mpya au la.  
  Reply by: dada neema, Date: 2010-07-21 00:55:55 [Report Abuse]    
     
  Dada Neema upo?jamani kina Janet, MamaE, Ke, aunt J, mamaB, tetea, passer by, Bro Dan, Mbwange, Doreen, Mama A-K, na wengine mliopotea mko wapiiii??? mpaka mpigiwe ramli ninyi?hebu rudini, itaneni woote huko jamani mrudi kha..kijiwe chawamiss huko rudini kwa speed  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-21 01:46:30 [Report Abuse]    
     
  Mimi kwa kweli dada Poleta nashindwa kukuelewa vizuri. Kama una kazi nzuri, kwanini usikae na watoto wako uwalee mwenyewe mpka ukae hapo nyumbani kwa huyo mumeo unayesema kuwa amekuwa mzinzi? Kwa sababu inaonekana kuwa mumeo hata watoto hawapendi ndio mana hata ada ya shule wakati mwingine hawalipii na anarudi usiku wa manane wakati watoto wameshalala. Huwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja, ndio mana naungana na wenzangu kuwa kama imefikia mahali ambapo mumeo anakuwa na mahusiano na wanawake wengine waziwazi, talaka hata kwa ndoa za kikristo inaruhusiwa. Kwa sababu hata huyo mwanaume mwingine hujatoa maelezo yanayoonyesha kuwa unampenda. Ninachoona hapa ni kuwa wewe unakosa sex kwa sababu hutaki kufanya na mumeo ambaye sasa hivi humuamini. Lakini mahusiano ya aina hii hayajengwi na sex bali upendo. Ninachokushauri ni kuwa usianzishe mahusiano ya kimapenzi na mwanaume ambaye si mumeo kwa kisingizio kujipoza na kumpoza kwa mambo mabaya yaliyotokea katika maisha yenu. Je kama ni usanii anaofanya tu ili mradi akupate. Kaa peke yako na wanao, hata kama kipato chako ni kidogo, watakula hicho ulicho nacho na watakua.  
  Reply by: mbwange, Date: 2010-07-21 01:59:16 [Report Abuse]    
     
  Da Maria n mbwange well said. POIROT kwa taarifa tu hapa ndani mara nyingi we deal with one sided story kwa sababu huo upande wa pili ni ngumu kidogo kuja hapa. Kwa hivyo basi tunajaribu kadri ya uwezo wetu kuangalia jinsi gani twaweza kumsaidia au tutoa suggestions kwa mtu mwenye tatizo kwa kuangalia pande zote mbili, upande wake yeye na upande wa mtu ambae analalamikiwa. Ikumbukwe kwamba hata JUDGE kuna wakati anatoa maamuzi bila kusikiliza pande ya pili hiyo kisheria inaitwa EX PARTE judgement, na hii inatokea ambapo upande wa pili hafiki mahakamani kwa sababu ambazo sio za msingi. KWAKO Poleta, nakubalina na wadau hapo juu waliosema kwamba si vema kuanza mahusiano na mtu mwingine ukiwa bado upo ktk ndoa. You should either sort out your issues na mumeo bila ya kuwa na mahusiano na mtu mwingine au uondoke kabisa na ndio uanze mahusiano na mtu mwingine. Na najua ngumu mno maana ku sort out issues lazima nyie wote wawili mume tayari kuongea. Ila naona kwa sasa mumeo hayuko tayari ku sort out issues, sasa hapo ndio ugumu ninao uona mimi. Sote tonajua kwamba in a relationship ku sort out issues lazima mkae kama mume na mke muongea japo mmoja hataki kuongea ni kasheshe maana peke yako you can not solve anything. Bongo naambiwa divorce mwiko, ila jinsi wewe unavyoishi na mumeo ni kama divorced couple ila yenu is not official. And i think that is the biggest problem you have ni kwamba YOU ARE LIVING TOGETHER BUT YOU ARE NOT TOGETHER. Cha msingi labda sort out problems na mumeo if you fail then make a clear decision on your situation. Mimi binafsi nisingependa kukwambia which decision to make but you should be as a adult be in a position to make a SOUND N WISE DECISION, for the future of your kids n your own happiness..-Ke  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-21 06:01:11 [Report Abuse]    
     
  maria nipo shost safari tu za kiofisi zinaninbana maana zimekua nyingi na natakiwa kuzimaliza b4 uchaguzi sasa nakosa muda kabisa nikipata ndio naishia kuchungulia nazip my mdomo, sikumojamoja ndo kama hivi natokea jumla. Kweli nammiss sana mama B na dada kemmy  
  Reply by: dada neema, Date: 2010-07-21 07:10:14 [Report Abuse]    
     
  Maisha bila mwanaume hayawezekani, kama ilivyo maisha bila mwanamke as well, mnapomshauri mtu jitahidini kuvaa uhalisia, JAMANI WATOTO WANAMLILIA BABA YAO, mnadhani hiyo ni kero ndogo? ama kwakuwa haijawakuta? Dada hustahili kuanzisha mahusiano mengine ukiwa na mume, ila kama ni kweli uliyohadithia ni dhahiri huyo mumeo kakuchoka aisee, hayo ndo maisha ya ndoa kwa walio wengi, inanishangaza ila ndo ukweli wenyewe, sasa cjui tufanyeje ili yaishe, halafu haya mambo ya mvurugano kwenye ndoa mara nyingi huanzisha wanaume, jaribu kuongea na mumeo dada na umweleze yote kuhusu watoto wenu, pengine atajirudi. Passer-by  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-21 07:14:03 [Report Abuse]    
     
  MIMI USHAURI WANGI NI MFUPI TU,KWA MUNGU HAKUNA LISILOWEZEKANA,WEWE KAMA NI MKRISTU,FUNGA NA KUOMBA KWA MUNGU,KAMA UNATAKA NDOA YAKO IRUDI VIZURI SALI SANA NA MKABIDHI MUNGU ,KAMA NI MUISLAM PIA SALI DADA YANGU ,MUNGU ATARUDISHA KAMA MWANZO,NA KUEPUSHA MABAYA,KUANZISHA MAUSIANO MENGINE WAKATI BADO UKO KWENYE NDOA YATALETA MABAYA MENGINE,LEA WATOTO MAMA,KWA KIPINDI HICHI FANYA MAZOEZI ITAKUSAIDIA KUPUNGUZA MATAMANIO.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-21 08:13:45 [Report Abuse]    
     
  shost, aka kwanini uumie hivyo,kisa kubembeleza mwanume, uvumilivu, ect. mbona wao hawatuonei huruma, babu wee nenda kampe huyo mzee chilo mliokutana nae, yeye hana time na wewe kwasabb anapakupunguzia minyege yake, atajiju kalianzisha nawe maliza kampe tu. midume mingi ndio zao wakiwa na visenti tu wanaunga cheni za mademu, nasi tujifunze babu ukichanganywa na mume or mchumba kama unavisenti vyako nawe tafuta viserengeti kwa elf 30000 unafanyiwa kila kitu na kunyonywa kwa bibi kwa rahazako, aka mwezenu siwezi kupata pressure kisa haya mavuvuzela, eti nizeeke mapema sivitaki mie, Monzela.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-21 10:53:10 [Report Abuse]    
     
  Naomba nieleweke inavyofikiriwa kuwa nimeweka “VISINGIZIO” vya kujirudisha au kuendelea kukaa kwa mume wangu. Unajua hata kama mimi nina matatizo na baba yao haina maana na watoto pia niwakatili juu ya mapenzi kwa baba yao.kusema kweli watoto wanampenda sana baba yao.siku anazoonekana nyumbani watoto huwa wanafurahi sana......Poleta  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-21 11:32:04 [Report Abuse]    
     
  Dada pole sana kwa matatizo uliyonayo. Sina mengi ya kuongeza, ila ni kama Da maria alivyoelezea hapo juu, sidhani kama ina make sense kuendelea kuishi kwenye uhusiano uliyokwisha vunjika eti kwa kisingizio cha watoto. Mie wakati mwingine huwa nashindwa kuelewa.. mtu anaposema eti kama sio hawa watoto mie ningeshaondoka.. Kwa hiyo inamaana ni watoto ndio wanaokuweka hapo si ndio?. Sasa dada angu unajua ni heri watoto wakaishi na baba wa kambo mwenye upendo, kuliko kuishi na baba mzazi ambae haonyeshi mapenzi hata kidogo. Effect yake psychologically ni mbaya sana ila wazazi huwa hatujui tu. Hebu kaa chini jiulize faida na hasara ya hayo maisha unayoishi kisha ufanye uamuzi sahihi. Huyo mumeo kwa mtazamo wangu hakutaki wewe pamoja na watoto wako. Kile kitendo cha kutokuja kuwaona ninyi kipindi umeondoka kilikuwa ni picha kamili. Hiyo ndoa yako imeshavunjika zamani sana. Fanya uamuzi wa busara acha kuumiza kichwa as if picha huioni.  
  Reply by: Daniella, Date: 2010-07-21 11:54:52 [Report Abuse]    
     
  yaani Da Neema labda wewe useme manake mie mamaB nimeshampigia kelele rudi rudi jamani hajaamua kurudi bado..Kemy sijajua nimefanyeje  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-21 13:48:18 [Report Abuse]    
     
  Poleta si umesema mwenyewe hata watoto kawasahau?, akirudi wamelala, kumuona kwa manati so what is the use..i think you are the issue here and not your kids..jamani akina mama tutatumia kivuli cha watoto kuvumilia abuse na vurugu hadi lini????mama hebu work on your issues, watoto wataelewa tu ingawa itachukua muda..offcourse separation au divorce sio jambo jema kwa kila mmoja..ila at times huna jinsi..watoto wana haki ya kuishi mazingira yenye nidhamu, upendo, amani..ambavyo kwa story yako havipo hapo kwako...so what is the use...  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-21 14:47:23 [Report Abuse]    
     
  NYAFURU & DANIELLA hebu jaribuni kwanza kuachika kwa waume zenu kwa miezi hata mitatu ndio mtoe maoni....hv mnajua mateso wanayopata watoto wanaoishi kwenye separated families??.mdada poleta as long as ndoa yako ni ya halali MLILIE MUNGU ATAIRUDISHA KUWA NJEMA KAMA MWANZO...hakuna ndoa nyepesi na MUNGU ANACHUKIA KUACHANA..na HAKUNA NENO GUMU KWA MUNGU...huko kwingine unakotaka kwenda utakutana na mazito...SIMAMA KWA NDOA YAKO NA TUNAZIDI KUKUOMBEA.  
  Reply by: dang, Date: 2010-07-21 15:32:02 [Report Abuse]    
     
  hivi Dang unajua mateso mwanamke anayoyapata kama anaishi na mtu asiyempenda? Nyamaza kabisa, hujui wengine tumepitia yapi...Mie kwa kweli wakati mwingine sionagi sababu ya kumlilia Mungu wakati naona kabisa hapa ninalazimisha mambo! Mungu nae ana mambo mengi ya muhimu ya kufanya..  
  Reply by: Daniella, Date: 2010-07-21 16:12:34 [Report Abuse]    
     
  Hivi kama asingekuwa na kazi nzuri mngemshauri nini? Tatizo linalotukabili waafrika ni kupenda kulalamika na kujiona ni victim. Laiti ningekutana na poleta ningemwuliza maswali mengi manake amejielezea kama malaika na hakuna jema lolote kutoka kwa mume wake. Minaamini binadamu yeyote hata hitler au osama(kama ni kweli yupo) ana mambo mazuri. Hivyo vijisenti visiwape kiburi, toa kwanza boriti jichoni mwako kabla hujamwambia mwenzio unakibanzi jichoni  
  Reply by: poirot, Date: 2010-07-21 16:17:09 [Report Abuse]    
     
  Hivi kama asingekuwa na kazi nzuri mngemshauri nini? Tatizo linalotukabili waafrika ni kupenda kulalamika na kujiona ni victim. Laiti ningekutana na poleta ningemwuliza maswali mengi manake amejielezea kama malaika na hakuna jema lolote kutoka kwa mume wake. Minaamini binadamu yeyote hata hitler au osama(kama ni kweli yupo) ana mambo mazuri. Hivyo vijisenti visiwape kiburi, toa kwanza boriti jichoni mwako kabla hujamwambia mwenzio unakibanzi jichoni  
  Reply by: Poirot, Date: 2010-07-21 16:20:04 [Report Abuse]    
     
  Poleta mpendwa mi nakuelewa sana ukisema upo kwa ajili ya wanao kwasababu najua nini thamani ya mzazi kwa mtoto. na mimi siku zote huwa najiambia lolote likitokea kati yangu na bb nitajaribu niwezavyo kulicontain ili mradi watoto wasimkose bb yao kwasababu mapenzi waliyo nayo kwake hata uwaeleze nini hawatokaa wakuelewa na yeye pia hawatamuelewa kwa chochote atachowaeleza kuhusu mm yao. Na daima matatizo yako na mumeo hayatakiwi kuwa kikwazo kwa watoto, hayawahusu. Watoto wana haki ya kukaa na wazazi wao. Lakini tambua kwamba unachofanya kina thamani sana mbele ya Mungu isipokuwa tu umesahau jambo moja, kumuombea mumeo abadilike! Najua hili la kumuomba Mungu linakwaza wengi na wewe kuendelea kuwa kwa mumeo pia ni kero kwa wengi. Lakini you are right kuvumilia kwa ajili ya wanao. Huenda watoto hawaoni km ni tatizo kwa wanajua tu hiyo ni life style ya bb yao. Kumbuka siku zote kukimbia tatizo sio kusolve tatizo hebu jaribu kwa kila namna uwezayo kutafuta suluhu na mumeo. Unanikumbusha mm mmoja ambae mumuwe alimtenda hadi akagawa nyumba zao walizojenga kwa jasho lao kwa vimada na hati akahamia huko akawa anakuja kuwasalimia watoto tu na kupotea tena lakini alipoanza maombi serious mbona mbaba alirudi mwenyewe kwa kutubu na kwenda kubadilisha hati alizokuwa amegawa huko, akajirudi, akapima maisha yakaendelea. Mm mmoja waziri wa serikali inayomaliza muda wake naye vilevile tena case yake ilikuwa worse lkn alisimama imara kwa sala hatimaye mambo yakaenda sawa. km wadau wanavyoshauri jitahidi kusali na kutafuta ufumbuzi wa matatizo yako na mumeo. Huko unakoelekea siko na tena wanaume mara nyiingine wanachukua advantage ameshaona you are vulnerable anataka kuku use mwisho wa siku akudump na kukuongezea machungu huenda hana hata tatizo na mkewe. Take care na nakuombea heri.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-21 16:22:21 [Report Abuse]    
     
  Reply by: Poirot, Date: 2010-07-21 16:20:04 .. Naomba nikutoe shaka uliza tu maswali yako, litakalokuwa ndani ya uwezo wangu nitakujibu...Poleta  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-21 18:25:59 [Report Abuse]    
     
  Dang unaongea kama vile hatujui nini tunasema, we have been there as kids, na kwangu kuna wakati najiuliza why should my mother go through hell ili tu nikae na baba?hivi mnajua inavyouma ukiwa kwenye ndoa ambayo mwenzio anarudi asubuhi, ana lala hovyo nje atakavyo, unaondoka kwa sababu yake , haji wala nini..then what are you saying people?na hakuna mtu kamwambia toka..yeye ndo muamuzi..ila kwangu kusema sijui watoto wamekwenda wamerudi haina nguvu..ndio watoto wanamtka baba yao..so ufe kwa sababu waione sura ambayo bado wanaiona kwa nadra..hivi hii maana ya kukaa na wazazi wote wawili ni ipi..mwili tu au tunapoongelea wazazi wawili tunamaanisha mambo mengi ambayo clearly hayapo..so ninyi mnaodhani wengine hatujui lets be objective on the issue..Dang bwana kwamba as long as ndoa ni halali abaki come on...jamani Mungu katupa akili ili pia itusaidie kupambanua mambo..na mie au Daniella kutoka kwa waume zetu ili kutaste what happens sio issue hapa..manake unataka kuiweka kama vile tunashabikia..kama mtu unanyanyasika kwenye ndoa ukabaki, baki kwa sababu wataka kubaki..tuachane na kusingizia watoto wakati bado tunawaweka kwenye mazingira magumu zaidi..so msidhani twaongea kwa sababu tumekurupuka.. na anabaki ili hawakautani kimwili, hawaongei, hawana mawasilino wala nini, mume kulingana na mada yake haonekani kama anataka maongezi au kurekebisha kitu..so why stay there, anyways wabaki sema nabaki Mungu nisaidie ila usiseme ohh wanangu....women tuna vizingiti kibao vinatuweka hatarini its high time kweli tufikirie tena, kuzaa haimaanishi utumwa..mie nina mtoto lakini there's no way nitanyanyasika ili tu yeye amuone baab yake kwa nadra..im still a human being pia..and kids need to respect that..na ninapoamua basi ni kwa jili yao pia sitaki wakae kwenye vurugu..i need them kuwa mahali penye amani..hakuna mtu anafurahia kuachika au kukaa mbali ila kama mwenzio analalamika huna haja ya kujiua..kwani ndoa alosema wanawake tu ndo wavumilie nani..jamani it takes two to make it work and thats the fact..anyways have fun na stay blessed kwenye hiyo ndoa kwa ajili ya wanao mdada..after all we are just contributing and you make the decision because its your life and you know better that we do  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-21 20:05:57 [Report Abuse]    
     
  I think marriage is a life time commitment ndio maana mtu akishaingia kwa yule anaeelewa alimaanisha nini kujicomit inamchukua muda kufanya maamuzi ya tofauti. Ndio maana watu wanahangaika kujaribu kutunza ndoa zao hata km zinagharimu maisha yao na bahati mbaya kina mama ndio wanakuwa vulnerable zaidi. Nevertheless tusi under estimate uwezo wa Mungu ktk kudeal na matatizo yetu ya ndoa kukimbia tu sio solution badala ya kukata tamaa mapema tujaribu kila jinsi kurekebisha hali iliyopo kwanza. Baadhi ya makanisa siku ya ndoa huwa kuna sala maalum kwa ajili ya kumuombea bibi harusi kwakuwa hata wao wanatambua pia kwamba mama ni msingi wa familia na mara nyingi anaaandamwa na changamoto nyingi na basi anahitaji msaada zaidi wa sala ili aweze kuzikabili changamoto hizo. Nadhani yameongelewa mengi hapa na wewe dada Poleta una majibu tayari imebakia kwako kufanya maamuzi sahihi. Katika kufanya maamuzi muombe Mungu akuongoze.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-22 01:03:43 [Report Abuse]    
     
  mm nataka kusema naomba dada waukweli hebu badili munekano wa hapo, mbele kilakukicha picha nihizohizo badili tafadhali niombi tu naona websate zawengine zinavutia kuremba kila mara tuweke hata picha ya vuvuzela basi kama huna zamatukio ya kila cku  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-22 10:23:42 [Report Abuse]    
     
  JAMANI HY NIMEWAMISS SANA,ni mimi wenu mumpendaye MAMA E,nipo huku "mtu kwao" ,mtandao situmii sana,eti najaribu kuishi kidogo bila internet lol!napumzika kiasi.Leo nimeona japo kwa simu niwaamkue.NIMEWAMISS sana da maria,janet,salua,daniella,elyc,Kisa,Kunda na wengineo wengi... Haya turudi kwenye mada, Poleta jamani pole,ila kwanini unakaa hapo?kufurahisha jamii kuwa tupo wote au?You are living a BIG FAT LIE dadangu,haumdanganyi mtu unajidanganya na kujipotezea muda wewe mwenyewe.unajua unawachanganya wanao namna hiyo,manake mpo tu mnaishi kama house mates.Kama imefikia hapo na hamna tena suluhisho,basi tafuta kwako ukalee wanao,mmalizane kabisakabisa,ndo ukishatulia usign mkataba mpya wa mapenzi.Ukianza uhusiano mwingine sasahivi,utaanza kuchanganya Chloroquine na Metakelfin,zote dawa za malaria.Utajioverdose dadangu,utakufa kihoro.Akijua tu mumeo una bwana,ataanza visa ataleta bibi yake hadi hapo home,itakuwa mashindano,mtakaowatesa ni watoto wenu.So,dada malizia kiporo cha kwanza,ndo uanze rasmi mengine. Wapendwa mwezi ujao nitarudi rasmi kwenye HY,mana ntakuwa nisharudi kule "kwa watu",kwa sasa wacha nimalizie holiday na kujaribu hii life without internet(stressfree) lol! Love you all! Its me MAMA E  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-23 14:54:12 [Report Abuse]    
     
  MAma E karibu sana, tumekumiss jamani haswaa. Plz pita pita huko uhakikishe umemleta dada Kemmy.. manake sijui nae ameshahamia ''kwa watu'', manake amepotea mnoooo  
  Reply by: Daniella, Date: 2010-07-23 15:31:43 [Report Abuse]    
     
  Mama E karibuuuuuuu, ehhe mwenzangu njema haswaa kujipa likizo na internet muda mwingine, hebu fun huko manake na mie nikikanyaga hiyo ardhi itakua balaaaa..karibu na huo mwezi basi umalizike haraka mama..love you tooo na weekend njema  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-23 20:10:28 [Report Abuse]    
     
  Mama E safi sana....have fun like there is no tomorrow. maanake ukirudi huku kwenye ulimwengu wa E utakuta stress zimepandiana utafikiri zimetumwa. Mdada mwenye mada, sijui unayaonaje maisha unayoishi sasa hivi. are you worth that life?ulivyorudi kwenye ndoa fake kwa ajili ya watoto, je unajitendea haki wewe na hao watoto wako? kama ulirudi kwa ajili ya watoto kwnini usiwabebe hao watoto ukae nao kuliko kujidanganya huko unakofanya? ni watoto wachache sana wataelewa hiyo sacrifice yako most of them watasema "...mum you had your chance for heavens sake...." si unawajua hawa watoto wa "dot.com" majibu yao yako kwenye template. as for a new relationshiop mimi naona usiharakishe. dont jump from one bad relationship to a stinking friendship. just take your time. chill my sister....tafakari ndio uchukue hatua!  
  Reply by: Pozi, Date: 2010-07-24 06:38:22 [Report Abuse]    
     
  Pozi well said mdada  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-07-24 14:21:43 [Report Abuse]    
     
  mmmh! ishu nzito. lakini mpendwa kama una kazi yamaana, gud and well endelea kutunza watoto mkishirikiana na mumeo. pili, kama muma anatoa matumizi nk apo nyumbani USIONDOKE! maisha ni kusaidiana mpenzi, ILA kama huyo baba ndo mmependana IBA lakini usijulikane, ukijulikana tu mwenzangu limekugeukia. mbona wanawake wa mjini ndo zenu siku izi? ila kama huyo baba anakuambia kuwa atakuoa muish wote ANAKUDANGANYA!!!! wewe kampime mmalizane haja zenu bai ila mambo ya kudanganyana eti oo nimekupenda mke wangu nilimkuta na mimba ya miezi 5 umehakikisha? unajuaje kama ni kambale doa? USEMEE MOYO WAKO unavyokutuma, yawezekana unaruka majivu unakanyaga moto au unaruka moto unakanyaga majivu, Akili mukichwa yako, jifikirie upya! mm naitwa bibi mzuri  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-27 02:50:37 [Report Abuse]    
     
  mbona mdada unataka kuanzisha yale ambayo yalikushinda kwa mumeo? I thought unataka kutoka kwa mume kwanza ndio uanze mahusiano mapya. kumbe wataka kuanza ukiwa humo humo! hapo utachemsha. kama una kazi nzuri, kipi kilikurudisha kwa huyo mume ambaye hata muda wa kukaa na watoto hana? siamini kama tabia ya mume inaweza kuwakosesha wageni. Wageni huja kwa ukarimu wa mke na si mume. wewe ungekua mwema japo hata wazinzi wenzie mumeo wangekuja, inaelekea hupendi wageni. malizana na mume then anza mahusiano mapya. ondoka, kalee watoto, utajichanganya tu wewe mwenyewe na kuongeza matatizo ndani ya ndoa ambayo inazama kwa sasa. watoto wanapata shida wakiwa na mama kama mama mwenyewe ni kiguu na njia na huna muda na watoto, lakini ukiwaweka karibu, wataishi vizuri tu. kote huko wengine tumepita, ni wewe tu bibie.  
  Reply by: Derby, Date: 2010-07-29 04:37:02 [Report Abuse]    
     
  dada kuna mawili hapo, sali na husiache kumuomba Mungu endapo utataka kurudiana na mmeo usikate tamaa la 2: kama ndio umekata tamaa n unavyoona na kufikiri kuwa moyo wako utaridhka ukianza uhusiano mpya then achana na mmeo,beba watoto kaanze upya...maaliza kiporo cha jana dada angu,mtaka mawili moja umponyoka..so uamuzi niwako.. FLORISH  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-07-30 15:57:08 [Report Abuse]    
Submit your comment here...!
  Topic IT'S MY STORY
  Reply
  Email Login/Register to use your username! (Click here)
   
  Enter Code
   
     
<<Back to Topics<< >> Reply to this message>><<EMAIL ME FOR NEW POST <<
womens pants, wedding dresses, wedding pictures, women shoes, wedding accessories, women nails, women hair, women message women send off, good wedding shoes and hotels
Any use of materials or photographs from HarusiYangu is strictly prohibited
© 2007. All Rights Reserved Designed and maintained by Bomba Designs