Home
About Us
Photo Gallery
Home
Planner
Planner
 
  TOPIC: How to move on

 

Wapendwa wa Harusi Yangu, natumaini wote mu wazima na MUNGU wetu mwenye upendo anaendelea kuwabariki. Tafadhali ninaomba mnisaidie, ninataka kumove on with my life baada ya kuseparate na mwenzangu kwa muda wa takriban miezi 5 sasa. Kisa kinachonifanya nifikirie kumove on ni kwa mwenzangu kukata mawasiliano kabisa na mimi sana sana akipiga simu ni kuulizia hali ya mwanae. (wenye kumbukumbu na kisa ya Doreen wairejee). Nilikuwa nimekaa kwa muda nikijaribu kumsihi tukae chini na kuongelea hatima yetu lakini amekuwa akikwepa bila sababu maalumu kiasi kwamba nimeshindwa kabisa kujua uamuzi wake. Nauliza nawezaje kuendelea na maisha ambayo kwa bahati mbaya yamesimama kwani siwezifanya maamuzi yoyote makubwa ya maisha bila kumshirikisha mwenzangu. Sasa kama haeleweki anachokiwaza au alichoamua na hataki kuonyesha wazi nifanyeje? Tafadhali nisaidieni.
  Topic by:Doreen/Norah09 Date: 2010-05-17   
       
  E-MAIL ME FOR NEW POST    
     
  Doreen pole sana dada. Mimi naomba kuuliza maswali yafutayo awali ya kutoa ushauri wowote: 1. What do you mean kwamba you can not move on or make decision without his permission or consent? 2. Je una kazi au una depend on him for your living? 3.Are you legally separated (mahakamani) or socially (kienyeji tu mmeamua kuachana)? Unisamehe kwa kukuuliza haya maswali, ila naomba unijibu ili nikuadvice accordingly...-CJ  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-17 03:58:03 [Report Abuse]    
     
  Da Doreen pole sana ns matatizo. Unajua kuseparate na mwenzi wako ni kitu kigumu sana. Ila hiyo reaction ya mwenzio ni kawaida kabisa ktk watu ambao wameachana..well akipiga anamuuliza mtoto wake which is fair enough, maana ugomvi upo kati yenu wewe na yeye na sio yeye na mtoto wake (so usimuingize mtoto wenu ktk ugomvi wenu). Tena shukuru Mungu kwamba anapiga kumuuliza mtoto wake. Labda jingine ni kwamba je analeta pesa za matunzo kwa mtoto wake? Maana hilo ndio jambo la msingi kabla ya kila kitu. Maana hauwezi mtu unamuulizia mtoto wako ambae hata senti hauleti. Na kuhusu kwamba kila jambo inabidi umuulize yeye mimi bado sijakuelewa hapo naomba ufafanuzi zaidi kama jambo gani? Vile vile anza kuzoea kwamba you are no longer with him. Which means you need to get used to it. Fanya mambo yako, kama kujiendeleza anza mara moja, na most of all keep yourself busy na sio kuwaza kwamba huyo ex mume hakutafuti. Yaani wewe inabidi ukae mkao wa kwamba if he calls sawa if he doesnt call sawa pia upo hapo? So jaribu ku invest muda wako mwingi ktk vitu vingine kabisa na sio huyo ex mume. Kama unafanya kazi wewe concentrate ktk kazi yako. Maana if you have decided to leave him-someone inabidi umuonyeshe kwa vitendo. Au una maana gani unavyosema yeye akipiga simu anamuulizia mtoto wake tu? So mdada kama umeamua kuwa mwenyewe jipanga dada na tena kumbuka kwamba huko dunia research zinaonyesha kwamba wanawake ambao divorced au single wanafanya career nzuri tu because thy are flexible..leo hii ukipata kazi New York wewe unaondoka ila wengi wenye waume wanaanza kupata discussion kubwa whether to go or not..so try to see the positive things on your situation sawa..ni ngumu ila jitaidi utaweza tu..na kama una elimu yako why not usitafute kazi nje ya nchi na upate Dollar zako shosti, na tena utakuwa mbali na huyo ex mume just a suggestion..all the best pray...-TX4  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-17 04:05:29 [Report Abuse]    
     
  pole, yawezekana wewe mwenyewe ndo chanzo cha mwenzio kuondoka "jino kwa jino" au kama sivyo basi tafuta namna ya kurudiana na mwenzio either kwa kuongea naye or kuwatafuta watu watakao waunganisha pamoja tena\ rose  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-17 04:35:01 [Report Abuse]    
     
  Mwathirika pole kwa hali unayokabiliana nayo,hiyo ndio mitihani yenyewe ya maisha ya Ndoa haswa za siku hizi lakini suluhu inaposhindikana basi hakuna jinsi zaidi ya kujitoa.Swali linakuja,sababu haswa ya kutengana ilikuwa ipi maana jinsi ninavyojua Ndoa za kikristu hazina talaka japo mambo yanaposhindikana kabisa mnaweza kupewa Utengano.Kuhusu kuendelea na maisha yako mwenyewe nakubaliana nawe na inawezekana kabisa japo itakuchukua muda kusahau na kurudi ktk hali ya kawaida maana matarajio uliyokuwa nayo kabla na baada ya kuingia kwenye Ndoa hayakutimia.Kwa upande mwingine nafikiri hii elimu nzuri na muhimu kwa vijana walio wengi kubadilisha fikra na mitizamo waliyo nayo kuhusu Ndoa.kwa muda mrefu muunganiko huu umekuwa ukitafsiriwa tofauti na kupotoshwa na kizazi cha leo kana kwamba yote yatokanayo na maisha haya ni ya kawaida tu.Hivyo suala la kudumu au kuachana ktkt Ndoa linachukuliwa kawaida tu maana limeshawakuta wengi.Na hali hii imechagizwa zaidi na watu wa rika fulani baada ya kushindwa kuishi Ndoa huku wakihubiri kwa mbwembwe wengine kuoana.Hivyo basi imebaki mazoea kwa walio wengi kuishi Ndoa tofauti na mpango na kusudio la Mungu linavyosema.Ni mtizamo wangu  
  Reply by: Mushobozi, Date: 2010-05-17 05:14:51 [Report Abuse]    
     
  mdau mimi sijakuelewa unavyosema´siwezifanya maamuzi yoyote makubwa ya maisha bila kumshirikisha mwenzangu´what do you mean? tunaomba ufafanuzi..MM  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-17 05:34:59 [Report Abuse]    
     
  Hata mimi mwenzenu sijaelewa bado anavyosema kwamba hawezi to move on with her life? Why?? Tupe mifano dada ili wadau wapate picha what you mean..ROSE mdau hiyo kauli yako ndio mambo tunayokataa hapa kila siku, ni aje tena ku judge huyo dada ..eti yeye ndio source ya separation..kila siku mke ndio course ndoa ikiharibika jamani hemu acheni hizo fikra za kizamani...-Ke  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-17 06:14:53 [Report Abuse]    
     
  Kama nakumbuka vizuri siku za nyuma doreen alisema anataka kuseparate na mumewe kwa kuwa matatizo ya kutoelewana kwao yalikuwa yamezidi kipimo. Alihitaji muda wa kuwa mwenyewe ili kusudi kila mmoja apate muda kuangalia wapi pamekosewa ili parekebishwe. Bahati mbaya sasa inavyoonekana mwenzie (mumewe) hayupo tayari kurudi ili kuendelea na maisha, na dada doreen labda amesha kaa chini na kuona umefika wakati muafaka wa kujua mbivu na mbichi, ndio anaona mwenzie haeleweki! ndio nilivyoelewa hii case. Sasa anaomba ushauri afanyeje tena, i.e next step...  
  Reply by: No email , Date: 2010-05-17 06:44:23 [Report Abuse]    
     
  Doreen samahani hata mie sijakuelewa vizuri una maanisha nini ukisema unashindwa ku move on au kufanya maamuzi makubwa mwenyewe bila mwenzio? kwani si umeshondoka kwa huyu bwana ? uliondoka mwenyewe au ulifukuzwa? kama uliondoka mwenyewe, ulikua na mipango gani, kuondoka ukapumzike kidogo halafu urudi au ulipanga kuondoka moja kwa moja? sijaelewa hapa. kama uliondoka kupumzika, nimekuelewa concern yako, ila kama ulikua jumla, then move on with your life, achane nae na msahau. kuulizia habari ya mtoto wake ni wajibu wake, hope na matunzo analeta. kama ilikua ni bishara ya kwenda kupumzika halafu anajifanya kuuchuna, mchunie na wewe uone atafanye nini in the end. fanya maamuzi yako mwenyewe, huhitaji kumhusisha mtu msioishi pamoja. mimi nimeseparate na mume wangu zaidi ya miaka 10 iliopita, sina talaka. but am happy the way I am, hakuna wa ku mbughudhi mwenzie, tuna watoto wawili naishi nao wote. kama hataki muafaka achana nae endelea na maisha yako. kama uliondoka kwa kero zake, haina maana kabadilika, he is still the same, kero zitaendelea.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-17 06:57:13 [Report Abuse]    
     
  Wapenzi samahani kwa kuchelewa kurespond. Nitajitahidi kujibu maswali yenu. Kuna waliouliza kisa au sababu ya kutengana- nadhani mkiperuzi kwenye topics za nyuma mtaona topics kama mbili zilizopostiwa na Doreen na ya kwanza kabisa inaelezea maisha yangu na mume wangu na hata kuomba ushauri juu ya nini cha kufanya nilikuja hapa. Samahani sitawezakurudia kwani ni mengi yalikuwa yamechanganyika. Pili kuna walosema inawezekana chanzo ni mimi mwenyewe, sikatai kwani najua hakuna perfect na mimi si mkamilifu lakini ukisoma visa vya nyuma mtawezajudge wenyewe. kuhusu kumwita na kuongea naye tumeshaitwa kwenye vikao vingi na kuwaona washauri wengi lakini haijasaidia kwa kuwa mwenzangu amekuwa mgumu na anaamini kuwa mimi ndiye mwenye makosa pamoja na kuwa wote tunaokaa nao wanamwambia alipokosea na inajulikana wazi kuwa yeye ana matatizo lakini nafikiri ni ile hali ya uanaume aliolelewa nao hajakubali to the extent that ameishia kuwanunia wote waliokuwa wanajaribu kueleza hali halisi including ndugu zake. Tatu ninavyosema nashindwa kumove on ni kuwa bado hatujaachana rasmi ingawa communication na intinacy hakuna sasa unapoanza kufikiria masuala ya personal development yako wewe mwenyewe ni lasima ahusike mwenza mf. kwenda kusoma nje ya nchi, kubadili kazi au hata masuala mengine ya kimaendeleo ambayo unajua kuwa yana implication katika hali ya uwili wenu.  
  Reply by: Norah09, Date: 2010-05-17 08:17:49 [Report Abuse]    
     
  Doreen i still dont understand why you should want to seek permission ya kufanya mambo yako ya maendeleo na mtu ambae hataki maendeleo na wewe. .mimi nadhani since you are separated fanya maendeleo yako mwenyewe na dont consider him as part of it. Maana hapa unachotaka kusema ni kwamba you are separated ila ukitaka kwenda kusoma nje lazima yeye asema yes?? Au eti ukitaka kubalisha kazi lazima yeye aseme yes?? Mhh aisee dada mimi naona unapotea sasa. Na implication gani hiyo ambayo utaipata ukingiendeleza nje, na trust me wanaume wa kiafrika tena eti unamuomba kwenda nje hapo atakwambia usiende na sio kwamba kwa mapenzi ili akukandamize tu. #Au leo hii utataka kununua kiwanja eti unampigia simu na kuuliza kama ununue? Aisee tena atakwambia nunua alafu weka jina langu (na wewe ndio unadhani hayo mapenzi kumbe ndio kutapeliwa huko)..wewe kama umeamua ku move on do it..njenga nyumba kwa jina lako, nunua vitu vyote kwa jina lako ect..maana inaonekana wewe unataka kuwa nae ila yeye alishamalizana na wewe siku nyingi..mimi naona wewe you should move on in the really sense...-TX4  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-17 08:27:05 [Report Abuse]    
     
  Kwa msaada kwa wale ambao hawajui mwanzo nendeni kwenye Topic posted on 30th November 2009 titled : Naombeni mnisaidie Tafadhali (kitu kama hicho) na ile ya tarehe 1st December 2009 by the title Special Message to Doreen. Nadhani mnawezapata mwanga kidogo.  
  Reply by: Norah09, Date: 2010-05-17 08:28:13 [Report Abuse]    
     
  TX4 kuna issue moja inafanana na hiyo mifano yako..mke na mume wame-separate (separation zetu hizi hizi za kienyeje za kibongo) ila mke yupo busy kumshirikisha mume ktk mipango yake (mume wala hashirikishi ktk mipango yake binafsi) ya maendeleo..eti kanunua gari na kumwambia mume, si mume akamwambia andikisha jina langu..mdada sijui akaona kwamba mume anarudi mbio kaandisha jina la mume..mume kashughulikia gari mpaka imetoka (si papers ziliandwa jina lake tangu huko Japan bwana), si na gari kaandikisha jina lake pia...tangu hiyo gari itoke bandarini mdada mpaka leo hii hajaiona hiyo gari mume ndio ameichukuwa na wala hana mpango wa kurudisha na si imeandikwa jina lake sasa utampeleka wapi??...mpaka leo hii analilia gari ambayo kalipia ila hajawahi kuendesha na anapanda madaladala..so wadada inabidi sasa mtulie na muanze kutumia akili za kuzaliwa..wewe mtu commucation mbaya hamna intimacy hamkai nyumba moja, kama ya huyo mume wa Doreen na still you feel kwamba maendeleo inabidi ufanye nae WHY???..sijui ila mdada uwe very careful..na kama unaenda nje kusoma mtoto si unamuacha na mama yako mzazi au ndugu zako full stop...kila la kheri...-MM  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-17 09:13:14 [Report Abuse]    
     
  Doreen jamani sasa utanifanya nikuchape kwa kweli..kwamba unashindwa ukitaka kubadili kazi unataka kujadili naye nini sasa wajadili hapo..nadhani kama mmeseparate manake mmejipa muda kila mmoja ajiangalie including kujaribu maisha peke yake..why do you need his permission mfano kubadili kazi manake wengine tuko ndoani lakini jamani sihitaji permission kubadili kazi..we just need to discuss na kuambiana sasa ni wakati ikitokea bahati nabadili kazi kwa sababu ya kadha wa kadha na sio ruhusa yake labda kama nje...napata picha hapa kwamba may be hujasema sasa basi..you dont want him out of your life yet, you are not sure kama umwachie au lah..mi kwa unavyoongea mwenzio alishakuachia au anaona unavyohaha so hana tena haja ya kureflect kila lililotokea na kujiangalia wapi alichangia manake anajua mwisho wa siku utabend..com on..move on...hebu acha kujali kapiga au hajapiga..angalia maisha yako na mwanao..na kama unapata shida ukipokea simu hakujali weka simu nyingine ndani na mpe number so he doesnt need to go through you unless kuna issue ya mtoto lazima muongeee..ni ngumu saana kuachana hata akiwa boyfriend manake ushamzowea na hujui waanzia wapi tena..ila hebu kuwa na courage jiambie unaweza my dear..mbona umeweza miezi mitano bila yeye?wasiwasi wangu ukiendelea wewe tu kufanya mazungumzo yeye anaweza kusema haya na turudi then cha moto utakiona..kwa sasa nadhani hajajifunza manake wewe unaadmit makosa yako yeye hataki means hana haja ya reconciliation yuko okay with or without you..hebu na wewe jiambie you can with/without him..he is just a man you met somewhere offcourse he is kind of differrent from any other guy in the sense mlioana lakini hataki sasa ujiue??????work on yourself kwa sasa, learn to be yourself, edit na ikibidi delete him from your definition of us ubaki na us meaning wewe na mwanao...jijenge upya, kama aje tafuta makazi mapya kama mmepanga..be positive..dont punish yourself tena..kama ulikosea jiambie ni ubinadamu na ujijenge ili ikitokea unakua kwenye uhusiano basi na uwe bora usirudie makosa yako..sali saanaa ili Mungu akutie nguvu..have fun, be with friends..ila muhimu love yourself na concetrate on you..Doreen na sio kingine tena..nimeandika gazeti manake bado nakumbuka hizo topic za mwanzo...hebu mama chanja mbuga..napata hisia the guy knows usivyojiweza na usivyoweza kuhimili chochote bila yeye...hebu muoneshe you can manake hukuzaliwa naye..muoneshe you had life beofre him and you can after him..usifanye chochote lakini kumkomoa fanya kwa ajili yako..dont try so much kuwa anione..do it for Doreen..then baada ya hapo sasa kama unaona giza bado then iwe permanent kama mwanga then you can work things out..ila kwa sasa nadhani mwenzio hayuko tayari na ondoa wazo la tukae chini tuongee au itatokea manake ukijipa matumaini utaishia kusubiri day in day out na itakuumiza milele...we only live once so make the most o it..sio crime mambo yakienda msivyotegemea ukaamua kujiondoa au mwenzio akajiondoa..ndo maana sie ni binadamu..so hebu fanyia kazi just Doreen na mwanao na sio ndoa  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-05-17 09:16:50 [Report Abuse]    
     
  dada zetu dada zetu...mhhh nitarudi baadae kidogo..-Mkaka  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-17 09:28:56 [Report Abuse]    
     
  Maria n TX4 kuleni 5 dada umechambua vizuri..inaelekea Doreen bado hana confidence kabisa kama yeye she can make it without him..pole dada you deserve better then this kwa kweli..fuata ushauri wa wadau...YEAR  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-17 09:42:03 [Report Abuse]    
     
  Wapendwa ninawashukuru sana kwa shauri zenu kwa kweli mmenipa confidence na nitayafanyia kazi. Hayo mnayoniambia nimeshayafikiria sana ila nadhani na nakiri kuwa uwoga wa jamii itanionaje na ile imani yangu katika ndoa ndio vilinifanya niwe muoga. But si kwamba ninamtegemea yeye kila kitu kwani hata wakati tu pamoja hakuna ambalo sikuwa naweza kulifanya. Nashukuru sana na ninamuomba MUNGU anitie nguvu. Lengo lilikuwa ni kujua how do I move on. Nina elimu ya kutosha na ninaamini si elimu ya kitabu tu bali hata uchambuzi wa mambo lakini kama wanavyosema wahenga mganga hajigangi, nakumbuka nimekuwa nikitoa ushauri kwa wenzangu katika mambo mbalimbali ya maisha including mahusiano lakini kwangu nimeshindwa so wapendwa nashukuru kwa kuwa sehemu ya Harusy Yangu family na kukutana na ninyi. Ninatamani sana nipate kazi nje angalau ya mwaka mmoja but sijui pa kuanzia. I am aware of the UN recruiting system na nimejaribu but nadhani MUNGU bado hajaamua na bahati mbaya ndio niijuayo so naomba mwenye ujuzi wa namna nyingine ambayo mtu anawezapata kazi ya aina yoyote nje anijuze. Aksanteni  
  Reply by: Norah09, Date: 2010-05-17 23:23:13 [Report Abuse]    
     
  karibu Doreen na Mungu akutie nguvu..na hizo kazi mama utapata..sometime it takes time Mungu kukupa anachoona kinafaa na uachohitaji..nakutakia baraka zoooote na amani tele..ama kweli mganga hajigangi na si mbaya kusikia watu wanasemaje it helps kuclear hali ya hewa na kukufanya ujue uko wapi...so tembea kichwa juu mama...na endelea ktafuta kazi hata yaweza kuwa hapo Tanzania lakini ikwa kila leo uko njiani so usijilimit kila jambo lawezekana.  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-05-17 23:43:53 [Report Abuse]    
     
  Aksante sana Da Maria kwa kweli umenitia nguvu sana ushauri wako pamoja na kuandika gazeti but hata nikishtushwa usingizini kuulizwa mstari wa saba wa gazeti la nyafuru unasemaje nina uhakika nitausema bila shaka maana nimekusoma na kukuelewa. Wadau woooote mlionisaidia ninashukuru. Mwajua woga wangu ulikuwa kwa vile hatujaachana rasmi yaani no talaka wala karatasi ndo nikajiona bado nawiwa kuwajibika kwake!! Jamani ni mengi nimepitia namshukuru MUNGU kunifungua na kunionyesha ninayostahidi.  
  Reply by: Norah09, Date: 2010-05-18 02:17:27 [Report Abuse]    
     
  Doreen i am happy for you that ushauri umekusaidia. Unajua we are all not perfect n we learning everyday through others. We understand that at the moment you a bit confused, desperate ect but remember those are only phases that will pass with time so have courage mungu atakusaidia. Cha msingi sasa kama wadau walivyokushauri sit down and plan for yourself a future with your child. Kuhusu kazi za UN kwa kweli ngumu sana kupata but kila mtu ana bahati yake so dont give up so easy endelea kuomba. Use the internet ili upata all the UN organisations. Mimi nina marafiki 3 wamepata kazi za UN na sote tulikuwa tuna apply pamoja na wenyewe wamepata ila mimi bado mungu hajanijalia. What I have learned ni kwamba usichoke ku apply hizo kazi. In the mean time work hard ktk hiyo kazi ulioyo nayo sasa. You must know that you blessed kuwa na kazi maana think of all the women who have no jobs na hata biashara za kufanya hawana ect. Otherwise good luck....-PJ  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-18 05:32:53 [Report Abuse]    
     
  me mbona cjakuelewa au?  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-18 05:51:00 [Report Abuse]    
     
  Doreen mengi yameshasemwa na wadau hapo juu, nimeumia coz you seem to hurting a lot, ni ngumu sana kuanza maisha mapya esp kama ulikua umezoea ya mwanzo lakini good news ni kwmba inawezekana. Nataka kushare na wewe kitu ambacho mimi kinanitia nguvu na kuona ukuu wa Mungu kila siku, ni hivi, jiulize ni kwanini simba jike ndie anaenda kuwinda na kuleta nyama wakati simba dume hafanyi hivi?na simba dume ndie anaeonekana mkubwa na mwenye nguvu?? wakati huo huo huyo simba dume yupo kwenye mabango yote ya utalii anatukuzwa na kuonekana yeye ndie yeye, wakati analetewa nyama na simba jike? it's funny coz ndivyo hata maisha ya binadamu yalivyo, mwanamke japo haonekani kama anaweza kumudu mazito na magumu lakini bado ana yahandle, anasonga mbele, anaenda kupigana na kuprovide kwa watoto wake, na mwanamme ukimuweka kwenye situation hiyo yako hata survive miezi miwili lazima atatafuta msaidizi, lakini cha ajabu wewe unaweza kuyaanza hayo maisha magumu mwenyewe. Point yangu ni kuwa Mungu ametupa sisi wanawake zawadi ya kipekee sana hapa duniani "uvumilivu" na tumebarikiwa na nguvu ya ajabu ambayo kiumbe mwingine hatoweza, YOU CAN DO IT MY SISTER, you have the power within yourself and you'll make it. Una nguvu ambayo hujui unayo Doreen jaribisha utaona. Nakutakia maisha mema mpz na hopefully utarudi kutupa positive feedback next time.  
  Reply by: janet, Date: 2010-05-18 09:54:54 [Report Abuse]    
     
  USHAURI WA BURE: Doreen mimi nakushauri ufanye maendeleo yako kwa siri sio lazima ajue au kama mdau Maria alivyosema usifanye vitu kwa kumkomesha mume wewe fanya vitu kwa ajili yako na mtoto wako ect wala fanya taratibu tu kwa raha zako tena kimya kimya...kama kiwanja nunua kwa jina lako na mwanao jenga taratibu..kama kazi tafuta utapata..na usiwe na pressure na mtu ambae anaonekana hana huruma wala mapenzi na wewe...sisi kaka yetu mtoto wa baba mkubwa nae alimfanyia mke wake kama wewe hivyo unavyofanyiwa ila kwa kweli sisi tulikuwa upenda wa huyo wifi yetu wadau muamini msiamini. Yeye alikuwa na watoto 3 na mume akachukuwa watoto kwa sababu kipindi hicho mdada alikuwa hana kazi nzuri. Cha msingi tukamwambia kwa kweli ajiendeleze,basi akasoma masoma ya jioni mpaka kapata degree (mind you huyo kaka yetu kwenda shule hakutaka kaishia form 6). Akapata kazi yake ya nguvu, na wakati huo watoto wake walishafikia 12 n 10 nadhani kamtafuta na sisi tukawaonyesha mama yao anafanya kazi wapi...si wakati huo ndio mume sijui kaishiwa..acha aanze kumtafuta..ohh tusaidiane kulea watoto mara ohh chukuwa watoto..hapo huyo kaka yetu kumbe kazaa watoto wengine 3 na huyo mke wake na wanaishi maisha ya taabu sana... Basi akawachukuwa watoto wake na wakapeleka ktk shule nzuri tu..na familia nzima ilimsaidia. Na watu wakamshauri kama anaweza aanze kujenga...kwa kweli kajenga nyumba kadogo na watoto wake, na maisha yake kwa sasa ni safi sana kwa anajiweza, na kwetu sisi yeye ndio wifi huyo wifi mwingine tunamuonaga kwenye sheria za kifamilia wala hatuongea nae...huyo kaka yetu bado anapanga huko sijui sinza vichochoroni...So mdada huu muda ni mzuri sasa ku concentrate ktk maendeleo ya kweli na sio huyo mumeo..USE THIS TIME DADA USIJEUKAJUTA HUKO MBELENI..Dada Zain  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-18 14:19:22 [Report Abuse]    
     
  Doreen una visa wewe eti hata ukishtushwa usingizini..manake umenifanya nicheke, thank you for making my night manake wanifanya nilale natabasamu..ubarikiwe mama  
  Reply by: nyafuru, Date: 2010-05-18 23:47:11 [Report Abuse]    
     
  Wapendwa naomba niuluze hivi ni nani aliyeanzisha wazo la Harusi Yangu forum??? yaani kwa kweli hamjui tu mlivyoliondoa giza lililokuwa limetanda moyoni mwangu yaani nilikuwa kila ikifika saa tisa usiku usingizi unakata na ninakaa macho hadi asubuhi wakati wa kwenda kazini yaani kwa kweli nimejitesa sana. Sasa ninawashukuru sana kwa ushauri wenu nimeshaanza mchakato wa maisha na ninaamini kabisa mwenyezi MUNGU atanisaidia. Mbarikiwe sana.  
  Reply by: Norah09, Date: 2010-05-18 23:53:14 [Report Abuse]    
     
  Nora09 hilo swali lako nadhani Administrator ndio muhusika mkuu atajajibu..  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-05-19 10:08:46 [Report Abuse]    
     
  NAUNGANA NA JANET MAWAZO YAKE NI MAZURI SANA KWANI DADA KAMA UMEFIKIA HATUA HIYO UNACHO OGOPA NINI?KUANZA MAISHA UPYA MBONA WANAWAKE MUNAWEZA?JIAMINI MUNGU ATAKUSAIDIA MAISHA YATASONGA LKN KABLA YA UAMUZI WOWOTE TENGENEZA MAZINGILA KWANZA  
  Reply by: WALCOTT, Date: 2010-05-28 07:36:26 [Report Abuse]    
     
  my dear i went thru that jamani acheni sio rahisi hasa kama unadhani there is second chance i have been separated like on year during all that time we fight, we make up we meet we spending sometimes together with our child like xmas, easter birthdays we even get back for several weeks during this time ok kwa sisi ni mama mkwe mtata anyways during all that time i knew the best thing is to get back together that is the best option doreen but i looked for a better job to suport my child and me and also now ninasafari ya kwenda uk kupata master yangu uk  
  Reply by: Anonymous , Date: 2010-06-01 08:48:28 [Report Abuse]    
Submit your comment here...!
  Topic How to move on
  Reply
  Email Login/Register to use your username! (Click here)
   
  Enter Code
   
     
<<Back to Topics<< >> Reply to this message>><<EMAIL ME FOR NEW POST <<
womens pants, wedding dresses, wedding pictures, women shoes, wedding accessories, women nails, women hair, women message women send off, good wedding shoes and hotels
Any use of materials or photographs from HarusiYangu is strictly prohibited
© 2007. All Rights Reserved Designed and maintained by Bomba Designs