Home
About Us
Photo Gallery
Home
Planner
Planner
 
  TOPIC: nahitaji mawazo yenu

 

mimi ni mdada niliyoelewa zaidi ya miaka mitatu iliyopita nina mtoto mmoja,mume wangu yeye nilimkuta akiwa na watoto wawili kwa mwnamke mwingine,nilimuomba mungu niwapende hawa watoto kama watoto wangu na ni kweli nilifanya hivyo ingawa nilikuta watoto wana behavior ambazo hauwezi ukapatana nazo hivyo nikasema ngoja niwabadilishe wawe kama watoto ninaowataka mimi kama kusafisha room yao,kuoga,kusafisha meno asubuhi,table manners,kutumia muda mwingine kwa kufanya kazi za shule badala ya kutumia muda wote kwa tv na other electronics game,nilipata vipingamizi kutoka kwa mume wangu mwenyewe kama vile nawafanyisha too much lakini ukweli wa mungu sikuwa nawafanyisha zaidi ya kutaka kama watoto wangu wawenilianza kuisha nao wakiwa na miaka 5 na 6 sasa wana miaka 9 na 10 lakini uwezi amini mpaka sasa bado wanatupa nguo chini,hawajui kuweka kwenye hamper/basket ya nguo chafu,hwajuhi kusafisha meza wakimaliza kula zaidi ya kutoa sahani yao na kuweka kwenye sink ata kuirinse kwa ajili ya kuweka kwenye dish washer most of time mpaka uwaambie.hawafanyi vizuri shule kila wenzao wakiwa na likizo wao inabidi waende shule mwezi mmoja kwa ajili ya kucatch up na wenzao.nikijaribu kuongea na mume wangu yeye anaona naongea kwakuwa si watoto wangu labda lakini ukweli ni kwamba ndani ya moyo wangu hakuna chuki hiyo ninaongea kwa ajili ya maisha yao.mpaka sasa ninavyoongea nikwamba ni watoto bado wakuwakumbusha go brush ur teeth,go take shower na ukumbuke ni wasichana.sasa hiyo ni cha mtoto mimi na mume wangu hatuishi kuargue for anything lakini mwisho wa siku baada ya mimi kukata tamaa na kuacha afanye anavyotaka yeye ndiyo anakuja kurealize what i argued with him ,i was right.wakati nipo busy kutake care watoto wake na kujua wamekula ,wameoga,wanalala pasafi,wamewahi school bus,wamefanya home-work na kuwatengeneza nywele yeye mwenzangu yupo busy na kazi na pia alikuwa anaenda shule kumbe mwenzangu kapata malaya mmoja ambaye alikuwa anenda kwa huyo mwanamke just having sex,na mungu si athumani bila ya mimi kujua huyo mwanamke akapata mimba na ni wa miaka 38 nafikiri alipanga ili alipwe child support na ili kuendelea kuwa na uhusiano na mume wangu,nimekuja kuambiwa baada ya mtoto anakaribia mwaka na mtu mwingine mume wangu alishindwa kuniambia na ni kweli muda si mrefu akapelekwa cortini kwa ajili ya child support na sasa analipa hiyo child support,sasa ndugu zangu ushauri ninaomba mimi ni kwamba nimemuambia mume wangu kwamba achague moja kati ya mimi au mtoto kwani siwezi nikaendelea kuhumiza moyo wangu kwa kuendelea kumuona huyo mtoto au mama yake.mume wangu akasema anajutia kosa na hataki kuniumiza tena hivyo alikubali kutokuwa na uhusiano na mtoto ingawa hiyo pesa ya child support inakatwa automatic,nimejaribu kuongea na huyo mwanamke nikipretend kama dada wa mume wangu na alikuwa ananiambia ukweli kwamba hawakuwa na uhusiano ilikuwa just for sex nikamuuliza ilikuwaje mpaka ukabeba mimba wakati wewe mwenyewe ndiyo unampigia simu na ukifahamu siku zako anakuja kukufanya siyo kwamba mnaenda out au what ni kwamba anakuja kukufanya tu,anasema ni bahati mbaya,nikamjibu bahati mbaya kwa dada wa 38 yrs old?sasa ndugu zangu nishaurini nifanye nini maana ni mengi siwezi andika yote,kwa kweli bado inaniuma inakaribia mwaka sasa tangu nigundue,simpendi mume wangu tena,i feel like he used me,ansema ananipenda lakini how can he cheat on me kama ni kweli ananipenda?na pia inamaana hakuwa ananifikiria mimi wakati anaenda huko ?pia huyo mwanamke sasa anasema anataka ampigie simu mume wangu akamuone mtoto,ingawa najua mume wangu hawezi kwenda kwani nilimuambia ndiyo itakuwa divorce yake.je is it ok kwa mume wangu kutoenda kumuona huyo mtoto?au nafanya dhambi?kwat what i blv product ya dhambi ni dhambi,pia hawa watoto wake niwafanye nini maana nimechoka fundisha sasa hivi nawasafishia room,nawapikia na kusafisha walipokula ata siwauridhi.na pia wananihita mama j nimewambia wasiniite mama j waniite kwa mya 1st name.je is it ok?maana leo wananihita mom ,kesho wakienda kwa mama yao ni mama j for two weeks then from nowhere mom again ,nimewaambia from today call me with my first name i don't want to hear mom,or mama j,je is ok?
  Topic by:kissa Date: 2012-06-13   
       
  E-MAIL ME FOR NEW POST    
     
  Mmmmmmmmmm mama pole sana kwa hayo yote. Kwanza bahati nzuri mimi ni mwanaume niandikaye hapa, na ninaishi huku ughaibuni.Kwa maelezo yako nimebaini kuwa pia wewe uko ughaibuni.Jambo ambalo uliingia kulifanya kuwasaidia watoto wajifahamu na wafahamu wajibu wao ni jambo la msingi sana. Watoto wengi wanaozaliwa au kulelewa huku ughaibuni ni mzigo mzito mnoooo!! Yaani watoto wanaharibikiwa hata kusogeza sahani au kupika chai tu mtoto wa miaka 18 utashangaa anasema hajui, hata kupika mboga au kufanya usafi hajui.Hadi wengine wameolwa hawajui kupika eti, wala kusafisha nyumba,ukiingia humo ndani utashangaa jinsi vitu vimekaa shagalabagala.Kwa hiyo ulichukua jukumu la maana sana kuanza kuwafundisha na kuwarekebisha watoto hao wakiwa katika umri mdogo.Kama mumeo hajakupa ushirikiano basi ni ngumu sana,na hasa kama siyo watoto waliozaliwa na wewe.Lakini usikate tamaa endelea kwani wako mikononi mwako wafundishe na wahimize kwa upendo tu.Mimi watoto wangu ni wakubwa kuliko hao napambana nao mtu hatoki asipoelewa kitu namwambia.Hayo majina ya kukuita mama J wafundishe jina moja la kukuita na nakuomba wasikuite kwa jina lako, wewe ni mama yao ni muhimu uwaambie wakuite mom si vinginevyo wakupe heshima yako. Juu ya suala la kumkataza mumeo asiende kumuona mtoto, mimi nadhani unafanya vibaya kwani huyo ni mtoto wake japo kamzaa nje huko lakini ni damu yake. Yaani hapo dada yangu usijidanganye kabisaaaaa maana hata umkataze ataenda kwani ziko njia nyingi atazitumia.Sidhani kama hilo ni suluhisho.Mruhusu tu na uwe huru naye.Unaweza kudhani labda hapo unazuia wasitiane tena, lakini binadamu utamzuia na mbinu nyingi tu mama!!. Mwisho nakuomba ukae na mumeo umweleze yote ambayo yamekusibu na mjue mnayaweka vipi ili ndoa yenu iendelee vema.Sijui kama ulijua siri ya kuachana na mke wake wa kwanza ulipokuwa unaanza kudesa naye huyo?Wakati fulani kina dada unaweza kuingia mahali fulani bila kufanya utafiti na ukifika hapo unaanza kuota joto la jiwe, na hasa huku ughaibuni wanaume wanasakwa kwa udhi na uvumba ili mradi mtu kapata mtu anaitwa mwanaume.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-13 13:59:42 [Report Abuse]    
     
  pole sana, kwanza mpeleke mkapime UKIMWI, kuhusu hao watoto achana nao hao ni PAKA PORI HAWAFAI, kama anaweza awapeleke kwa shangazi yao, au bibi yao. Hata kama unawafanyia nini, bado hawatakuelewa, siku ya siku watakutukana na wataondoka zao.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-14 00:19:35 [Report Abuse]    
     
  mmmh we Anonymous , Date: 2012-06-14 00:19:35, yani kwa maelezo yako hadi umenitisha unaonekana huwezi kabisa kulea mtoto wa mtu mwingine, ndo wale mama wa kambo wenye roho za ajabu. Angekuwa mwanao ungesuggest awe treated hivyo unavyosema? swala la watoto kushindikana si tu kwa kuwa wanalelewa na mama wa kambo, hata mtoto wako wa kumzaa anaweza kukushinda tena nimeshaona wengi sana, ila kitu ambacho nimegundua sisi wanawake tuko so quickly kuhukumu watoto wa wengine, tena unakuta mwingine yuko busy kumsema mtoto wa mwenzie wakati wakwake ndo worse zaidi. Tubadilike kwa kweli tuwe na upendo wa Mungu usio hesabu makosa, na wenye uvumilivu especially kwa watoto. Dada ulieleta mada unaonekana una roho nzuri, sema tu mumeo ndo anaekuangusha, Muombe sana Mungu tena kwa kufunga ili akuonyeshe njia, unajua kuna mambo mengine hayawezekani bali kwa kufunga na kuomba tu. And more important dont giveup on those children, tunaambiwa tuweke hazina Mbinguni na si duniani, na usisubiri wala kutenda kwa kutegemea shukrani za binadamu, wewe Tenda bila kuchoka huku ukimtumaini Mungu na malipo kama si duniani basi Mbinguni lazma utayakuta ambako ndo nyumbani kwetu kwa milele hapa duniani tunapita tu so it doesn't matter much kama binadamu wenzetu wanatulipa au wanatuchukuliaje. Gudlucky  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-14 01:22:04 [Report Abuse]    
     
  AKIAMUA KUFUGA PAKA PORI KAZI KWAKE, HANA MSAADA WOWOTE, HATA PANYA AKIPITA HAKAMATI, HATA UMPE CHAKULA GANI HANA SHUKRANI, UKIMPA MAZIWA. SOSEJI, KABABU, CHAKULA CHA WAHINDI, WACHINA HANA ASANTE, AKIPATA.............. UPENYO.... TUU.......... LAZIMA............. ARUDI POLINI........................, USHAURI WANGU ACHANA KUCHANYA PAKA WA KAWAIDA NA HAO WA POLINI. MBONA UNAKUWA NA HURUMA ZA AJABU AJABU. VIJITU VENYEWE HAVINA FAIDA  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-14 02:44:20 [Report Abuse]    
     
  GODLUCKY WE MTU WA AJABU, YAANI UNA MSHAURI AWE NA UVUMILIVU KWA AJILI YA PAKA PORI, AFANYE MAOMBI KWA AJILI YA PAKA POLI, ACHA MASIHALA, HAWAFAI KABISAAAAAAAAAAAA HATA KUONA MACHONI. WARUSHENI PORINI SIKU WAKIWA WAKUBWA WATAKUJA WENYEWE HUKI DUNIA IKIWA IMEWANYOSHAAAAAAAAAAAAAAAAA  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-14 02:55:03 [Report Abuse]    
     
  Dada mtoa mada kwanza pole sana kama ni kweli unayosema yataka moyo na utulivu wa kutosha yaonekana kosa lilikuwa toka mwanzo wa mahusiano yenu wewe hukuweza msoma mapema huyo bwana tabia yake ukajiingiza kwenye mahusiano siyo pia kwa mtazamo wangu yaonekana hukuupata ukweli halisi hasa uliomfanya waachane na huyo mama wa watoto wake hapo kilichokuwepo wewe endelea kuvumilia na kwa huyo baby mama wa pili hata ukimzuia kwenda huko ni bure kama jamaa ni tabia yake hawezi kuacha wewe mpe free way kwenda muona huyo mtoto wake maana tayari kisha unga undugu huwezi kumzuia cha msingi tu jua hapo ndoa imebaki yako pekee yako si kwa huyo bwana tena sahau kwa sasa nakuomba kama wewe mkrito kuwa mtu wa maombi kwa sana kama muislam kuvuta msala kwa sana maana Mungu ni mwema kila kilicho na mwanzo kina mwisho as kwa hao watoto kaa nao endelea kuwapa upendo kama wa mwanzo jaribu kucontrol hasira zako juu ya huyo mume kutokupelekea wewe kuwachukia watoto kwa sasa kaa kimya hao watoto wakike wakishavunja ungo mshauri mumeo awapeleke kwa mama yao maana kwa kipindi hicho ndicho kigumu zaidi watahitaji kuwa karibu na mama yao kuliko mtu mwingine na ukizingatia kila usemalo au utendalo juu ya hao watoto unaonekana sivyo ndivyo kwa kuwa tu watoto si wako unajua watoto wa kike wakishakuwa wanapendeza kuwa karibu zaidi na mama yao hasa wakisha kuwa wamevunja ungo na watoto wenyewe wa pande mbili huwezi jua upande wapili yeye atakuwa analichukuliaje na kumbuka kuwa mama ni mama tu isije ikatokea ukaeleweka vibaya pindi watakapo kuwa na kuanza kujitambua.Kila la heri mtangulize mungu kwa kila jambo.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-14 03:14:24 [Report Abuse]    
     
  Bi dada unataka hao watoto wanyooke ili iweje,mtoto wa fisi ni fisi tu hata ufanyeje mifupa ni yake tu, unataka uwanyooshe ili waje wakusaidie nini wewe, huwezi ukabadilisha atittude yao kwamba wewe si mama yao na mumeo atazidi kukuona unawachukia,hebu jikite kwenye kumnyoosha wa kwako ondoa rabsha. Pia huna haki ya kumkataza mumeo chochote juu ya mwanae mwingine, kwani mchezo ni ule ule alioufanya kwa mama wa hao watoto, na ataendelea kufanya hivyo kwa kutaka huyo mzee aje amlelee wanae .  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-14 08:10:19 [Report Abuse]    
     
  Pole Kissa. Maelezo yako marefu hivyo sijasoma ushauri wa watu wengine hivyo kama nitarudia unisamehe. Mimi nimeishi na ndugu wa kambo (mamangu aliolewa na mwanaume mwenye mtoto pia). mamangu alijtahidi kumuweka yule mtoto kwenye mstari lakini wapi. Alikuwa hapendi kukaa nyumbani, mdokozi, shuleni hafaulu, wakati mwingine hafiki shuleni mamangu ndo anaenda shuleni kufatilia kesi zake, muongo, yaani mtoto mbaya. Malipo aliyopata mamangu ni lawama toka kwa mumewe, ndugu za mumewe na baadhi ya majirani na aliishia kupata ugonjwa wa moyo. Nilichojifunza pale na kwa wengine na kwenye maandishi ni kuwa MTOTO WA KAMBO NI WA KAMBO SI WA KWAKO. Hivyo basi unatakiwa we ujue kuwa huwezi kuwa mama mzazi wa wale watoto na wao hawakuchukulii kama mama yao. Hiyo bond imetoka wapi? Mtoto wa kumzaa ukimchapa anaona ni adhabu na soon akimaliza kulia anakurudia maisha yanaendelea. Mtoto wa kambo ukimchapa umemuonea kwa kuwa we si mamake! Inatakiwa watambue wewe ni mke wa baba yao na si vinginevyo. Manake ni kuwa usiingilie mambo yao na hasa kuwahimiza vitu na kuwaadhibu. Hiyo kazi mwachie baba yao. Jenga mahusiano nao taratibu kama unavyozoeana na watoto wa jirani zako. Hata siku 1 usivae viatu vya mama. Kwanza wanakuchukia kwa nini uko pale na si mama yao. Ukambo wao tayari ni silaha ya ku-win sympathy ya watu wengine hasa baba na wanaweza kabisa kukufanya ukimbie ndoa. Mi nakushauri uachane nao kwa muda:waoge wasioge, wanye kitandani au chooni we waache ila usiwanyime chakula. Mengine waache kabisa hata kama watapinda usiogope lawama maana hata sasa unalaumiwa. Roho itakuwa inakuuma lakini kuna kitu utakuwa unajenga ndani yao. Nimewahi kusoma article 1 watu walioshi na mama wa kambo walikuwa wakitoa experience zao. Mmoja anasema alikuwa akimchukia sana mamake wa kambo na wakati mwingine alikuwa akimsingizia uongo kwa babake. Yule mama alikuwa akijitahidi kufanya mambo mengi kumfurahisha lakini alikuwa hamjali. Baadae yule mama alikuja kufa na huyu binti anasema anatamani akafukue kaburi amuombe msamaha yule mama kwani hajawahi kuona mtu mzuri kama yeye. Ishi nao kama binadamu wenzio na taratibu watakuheshimu. Kuhusu majina inaonekana kama hilo la mummy wanalazimisha kwa kuwa unalazimisha kuwa mama. Tayari wana mama hata kama marehemu. Baadae wakijiskia watakuita. Hilo la mumeo kuzini na hatimaye kuzaa halimaanishi kuwa hakupendi. Ni tamaa zake tu na asingezaa usingejua hivyo usingeweza kusema kuwa hakupendi. We kasirika, lia ukiweza, fanya chochote ku-relieve hasira na uchungu ila usifanye upuuzi zaidi. Tumia busara zaidi. Siko kwenye moyo wa mumeo lakini naamini hata yeye hafurahii yaliyomkuta. Kuhusu mumeo na mtoto mpya hilo huna budi kulivumilia tu dadangu. Mwache mtoto na babae. Ni bora aende kwa uwazi kuliko kwa siri maana utaumia zaidi ukijua. Aamue mwenyewe kutokwenda ila si kwa shinikizo lako. Afterall huyo mwanamke ameshazaa na mumeo ataka ngono tu, so huenda akatafuta mwanamke mwingine ambaye hana majukumu (sikutishi) najaribu kuondoa hofu yako juu ya huyo bibie. Hakuna ndoa isiyo na madhila ila kudumu au kuvunjika hutokana na namna mnavyoyachukulia/kutatua matatizo. Ukiazimia isivunjike na mumeo akaazimia hivyo hakika mtadumu na huenda mkawa na furaha zaidi huko mbele kwani mtakuwa mmeweza majira ya mitikisiko. Nakutakia kila heri, take your time, do not take husty decisions puliiz. LUKUNDO  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-14 09:53:26 [Report Abuse]    
     
  LUkundo, Umeongea ya maana nimekupenda sana. Mimi ni mwanaume na sijapenda hali ya huyo mwanaume mwenzangu, lakini pia wewe mdada huhitaji kuchunga mwanaume mwachie huru kwa sababu ukichunga atatafuta njia ya siri ambayo ndio itakuwa na madhara makubwa zaidi.Kama Lukundo alivyosema,naamini mumeo anajutia moyoni kwa hayo aliyoyatenda japo hawezi kukuambia bayana.Mpende ongea naye kwa upendo kabisa kama vile hakuna kilichotokea mrejeshee ule upendo wa tangu mwanzo kuwa karibu naye mtulize, utaona mabadiliko.Lakini ukizidi kukasirika utazidi kumfukuzia mbali.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-14 10:01:17 [Report Abuse]    
     
  nashukuru kwa ushauri.mimi namuamini mungu na siku ya mwisho,hivyo najitahidi kuishi maisha ya kumpendekeza mungu ili kesho nisije juta kwa mungu wakati nilikuwa na nafasi ya kufanya hivyo.kwakweli sioni future na mume wangu kitu kinachonifanya niwe naye ni assets ambazo ziko nyumbani kwetu mimi nchi/ambapo nikiachana naye yeye hataweza kuzimiliki.ata kidogo na sipendi dhambi ya dhuruma.kusema ule ukweli mimi siwezi kucheat kwani ata nikienda kwa mwanaume mwingine siwezi enjoy kwani mawazo yatakuwa kwake kwanini namfanyia hivi na pia najua roho itanisuta,hivyo najiuliza how come he did it?ata hakunifikiria mimi ata kidogo?baada ya kugundua nilimuambia acheck STD,na alifanya ni kweli anajutia na anapologolize lakini mimi bado nakumbuka when i tried for my level best to be good mom yeye anafanya alivyofanya.kuhusu huyo mwanamke alikuwa anasema yeye hajali kuwa na mtoto ambaye baba yake hana habari naye lakini sasa naona anajali kwani anataka akaone mtoto,mimi sitaki na sitoruhusu kwani nataka nayeye mwanamke afeel the pain which i went through with,alikuwa anajua mume wa mtu,hawakuwa na uhusiano wa kwenda out or what just for sex,na ni yeye ndiye alikuwa anampigia simu mume wangu aende nyumbani kwake akamfanye ,na yupo over 37 anajua siku zake,so to me she just planned so that she will still see my husband kwa njia ya mtoto,hivyo i wanner punish her to have baby in 36yrs and her dady doesn't care about the baby.now i think it works because she started to think about calling him to go over and see the baby,last nimemuambia mume wangu akithubutu kwenda kuonana naye na nikija kugundua even after 5 yrs I will file for devorce. KISSA.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-14 11:01:30 [Report Abuse]    
     
  Pole sana dada Kissa. I can imagine what your going through. Mimi wangu alichiti lakini nashukuru hakuacha muhuri(hakuzaa) lakini sasa ni mwaka karibu wa tatu nikikumbuka nahisi BP inapanda (wakati wala sina hiyo BP) Jamani kuchitiwa kunauma hasa kama wewe ni faithful. Yani mbaya zaidi nilimjua alochiti nae; basi wakati mwingine najisemea ningekuwa na pisto ningeua . Eeh Mungu nyie wanaume mtatufanya tunyongwe kwa urder case. NI ngumu, ngumu sana kusamehe na kusahau. Na hiyo ndiyo inaharibu kabisa ndoa kwani waweza ukawa unalia hata miezi sita mfululizo; nambie; tena hata kwenye sex unahisi kama unabakwa. Mi bado kidogo nidai talaka kwani nina uwezo wa kumudu maisha na wanangu. Lakini Mungu wa rehema, alinipa ujasiri, najitahidi nisahau. Nyie wanaume jifunzeni kufunga zipu zenu; mnatutesa. Hao wanawake husband snatchers sina cha kuwashauri kwani wao by nature ni watu wenye roho mbaya ambazo hata ufanyeje huwezi zibadili. Wanatuambia tu deal na waume zetu, ndio misemo ilozagaa mjini. Sijuhi tu deal nao vipi???  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-14 17:48:47 [Report Abuse]    
     
  pole sana kissa suala hili ni gumu sana kuliamua kwa haraka kwani ya kesho hakuna ayajuaye leo wanaonekana watoto ni paka poli kwa ajili ya dhambi ya wazazi keshokutwa wakifanikiwa ktk maisha sijui misaada yao nayo itakuwa paka poli mie naona watoto wasiwachonganishe wakati mnatafutana hamkuwahusisha.nenda naye polepole huyo mzee ataelewa tu. pia tafuta kitabu kimeandikwa NDOA NI KUKAZAMOYO kitakufariji sana.Wallcot  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-15 02:14:16 [Report Abuse]    
     
  pole mwaya kisa., mim sijaolewa na sisemi mtazamo wangu ni sahihi .. kwenye mapenzi kwangu ni full kupendana inapofika mpaka kucheat na ten tena nikajua mpaka na mtoto umezaa nje .. aiseee hakuna msalie mtume .. nakuacha hata kama tutakuwa tumezaa watoto kumi , NAKUACHA hata kama ndoa inasiku mbili tu naivunja, no kuvumilia .. oky unavumilia mpaka lini??? and why unavumilia .. is not guaranteed kwamba atabadilika ... let have confidence bana , yani alikulete wa wawili ukawakubali na baada ya wakwako amekuletea mmoja.. eehhhhh ehhh sijui labda mimi sijui kupenda , nakuacha na watoto wao nasepa na wakwangu kuanza a new life .. very new unajua mpaka watu yatukute makubwa ndo tunajua kuwa tulikosea, ila kabla ya makubwa viashiria vipo bwan kwann mtu unganganie mume??? take your shoes no tyme mama anza mbele..marriage is not for everyone!  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-15 02:42:03 [Report Abuse]    
     
  nimejifunza mengi kwenye hii topic. nakupongeza sana kissa kwa moyo mzuri ulionao wa kulea watoto wa mwanamke mwingine kama wanao, wanawake wengi hawana huo ujasiri na examples umeziona kwenye comments hapo juu. i cant imagine mtu unadiriki kumwita binadamu mwenzako tena mtoto eti paka pori! nimeumia sana wadau its sad and bad. put your child on that shoe aitwe paka pori how would you feel as a mother au labda wenzetu hamjabahatika kupata tumbo la uzazi sad really. Kissa pole kwa yaliyokukuta kwa mumeo . LUKUNDO i salute you for your comment umenipa elimu ya hali ya juu sana kuhusu swala zima la malezi ya mtoto ambaye asiye wako. kissa endelea kusimama imara kama mama na muhimili wa familia. hakikisha hautetereki kabisa. watoto na mtu yeyote atakayeishi katika nyumba yako aishi katika misingi uliyoiweka wewe. labda angalizo tu be fair at all times and treat everychild in the family equally kama ambavyo unamtreat mtoto wako uliyemzaa. watu wengi wanapenda wafanyapo jema wapewe fadhila duniani tunasahau kuweka akiba katika benk zetu mbinguni so Kissa fanya kile unachoona kinampendezesha mungu machoni pake na siyo mwanadamu katika malezi ya hao watoto. i believe mungu amekupa huyo mume akijua kwamba utaweza kukabili mitihani yote ya ndoa ndio maana nikasema simama imara na usitetereke. hao watoto wakikua wasipokuthamini kama mama usijali jali kile ambacho umekifanya sahihi end of the day utasema you played your part na wala usiache just because dad sijui hapendi. take those kids as watoto wa mtu yeyote yule such as wa kaka yako dada zako nk je ukiona hawaendi kwenye mlolongo unaostahili utawaacha? keep maintaining the standard kwamba mpaka watakapofika age ya kujitegemea and as long as they live under your roof they will live under your rules thats it. mumeo kucheat na kuzaa nje my dear its a challenge sababu i know you wish to break that bond ya mumeo na huyo mtoto something which is impossible na tena ni dhambi sababu huyo mtoto hakuchoose kuzaliwa katika hayo mazingira. cha kukushauri mbane tu mumeo na be straight to him and continue to maintain kwamba asiende kwa huyo mwanamke kumuona huyo mtoto but rather kuwe na arranged plan ya jinsi ya baba kumwona mwanae be it awe anamchukua na kukaa nae hapo kwenu for a day or specifi days but cut off him kwenda huko na be open to that lady now come to the surface as his wife ikiwezekana basi uwe unaenda na mumeo kumwona huyo mtoto. ila bana him sana atleast apunguze uhuni.kumwacha siyo solution maana naamini hutaweza ishi peke yako bila mwanaume for the rest of your life and your not guaranteed utakayempata atakuwa faithful pia statistics ( atleast za bongo) proves 95% ya wanaume ni cheaters sema wanatofautiana degree of cheating wengine wako to the extremes wengine ni biginners. PRINCESS  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-15 02:42:49 [Report Abuse]    
     
  Pole sana Kissa kwa unayoyapitia. Kwanza ninachitaka kukukumbusha ni kuwa watoto wote wako hivyo kwa maana wanahitaji kuambiwa na kufundishwa tatizo ni kuwa kwa vile si watoto wako wa kuzaa inakuwa vigumu kuchukua hatua madhubuti katika kuwaadibisha maana unamvutano kati ya mumeo anaona si sahihi kuwafundisha na kuwalazimisha kwa vile hukuwazaa lakini naamini hata wa kwako ungewafundisha hivyo hivyo na ingekua rahisi maana hata fimbo ikibidi utawacharaza ili kuweka akili zao sawasawa, lakini sasa hawa watoto wa kambo inakuwa ngumu saa nyengine kuchukua hatua madhubuti kwa kuhofia huko muliko na sheria za huko mtazamo na pingamizi ya baba yao kwa kisingizio anawalinda dhidi ya mateso ya mama wa kambo, Ninachokuomba usikate tamaa kwanza jaribu kuwa marafiki na wao pia wakumbushe bila kuchoka unapoona wamesahau au hatataki kufanya kama unavyotaka watakuja kukuelewa baadae hata kama hupo duniani, fanya wajibu wako na mungu atakulipa kwa wakati wake. Waeleze sababu ya wao kufanya hayo ni kwa sababu wanatakiwa wakue ili wajiandae jihudumia na kujitegemea. Kuhusu mumeo naona unasababu maalumu ya kuendelea kuwa nae, na hiyo inaashiria upendo bado unampenda ndio maana unauwezo wa kuvumumilia na kuhofia kumharibia, ninachokwambia ni kuwa amani ya moyo wako itaamua juu ya hili maana upime faida na hasara utakayoipata utakapoachana nae na kuona huyo mama mtoto mpya kashika ukanda akifurahia furaha uliyokuwa unaipata kwa mumeo. Si kama nakusimanga au nakulazimisha ila nahisi bado unampenda mumeo na hiyo ni kawaida, jipe moyo onyesha upendo huo kwa mumumeo unaweza kumrejeza na kuona kwa nini anakufanyia hayo lakini bado upo pale. Mkumbushe kuwa awe makini na maisha ya sasa si vema kudondosha watoto nje kisha akuletee wewe ulee. Pole sana. Salua  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-15 03:21:54 [Report Abuse]    
     
  mwambie baba yao kuhusu watoto wake, wanakuwa na soon wataanza kujitegemea na wanaweza kuolewa,awabadilikie, bila support ya mumeo kwa hao watoto utaendelea kuumia. km unaona hiyo action uliyoichukua kwa mumeo itakupa faraja, ni sawa. kwani in any way lazima ureact kwa kitendo alichofanya mumeo. wengine tulijifanya kukaa kimya as if nothing happen na mume anaona maisha yako poa, kumbe mwenzie napanga revenge ya kumuacha any day kimya kimya, which is very bad kwani yeye anajua niko poa na nimesamehe. so km unaona kumkataza kwenda kumuona mtt ni faraja kwako na unajisikia vizuri na ni njia moja wapo ya kumsamehe endelea tu. najua machungu ya mwanaume kucheat na kuzaa nje ya ndoa. imani na mapenzi vinakwisha kabisa, kaza moyo react jinsi unavyoona ila tu usiwanyanyase hato mabinti zako. kila la kheri.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-15 09:08:40 [Report Abuse]    
     
  Salua, Lukundo, na Princees, wamekushauri vizuri na naamini utaweza kuchambua hayo mema ya kuyashika. Unajua dawa ya moto ni baridi.Na dawa ta baridi ni moto. Hapa namaanisha huwezi kumrekebisha au kurejesha tabia ya mumeo kwa kulipiza kisasi.Kama wewe ni mwaminifu basi usivunje uaminifu wako, yaani bado jihimize kumpenda na kumwombea na kumtaka ajijue ili uwe pamoja naye.Kama mwanao kapata mimba nje ya ndoa, halafu mzazi unamfukuza nyumbani, maana yake unazidi kumpotezea mwelekeo. gari likiwa bovu huhitaji kulipeleka barabarani,bali linahitaji kupelekwa gereji litengezwe kwa sababu unataka uendelee kulitumia vizuri. Najua jinsi unavyoumia kwa hayo yaliyojiri na mumeo,lakini hatujui pia mapungufu yako wewe kama mwanamke. Legeza kamba na mpe ushirikinao mumeo nenda naye kumuona huyo mtoto au wamlete nyumbani kwako ake naye masaa kama mko karibu. Kuhusu malezi ya watoto uliowakuta na mumeo, nadhani watoto wengi wanakuwa hivyo, hivyo kitu muhimu ni kuvumiliana nao,na wala usiweke kitu katikati kwamba ni kwa sababu si watoto uliuoazaa wewe, hapana,endelea kuwahimiza kuwa watoto wzuri na kuendelea kupendana nao. Kuna watu humu wamewabatiza hata kwa majina mabaya kama"Mbwapori" nadhani wengi wanashauri humu wakiwa na hasira ya mambo yaliyowakuta au ndo malezi walioyapokea kwa wazazi wao. hakuna mtoto asiyeweza kurekebika.kama wengine walivyosema, kwa mtoto mdogo si rahisi atambue kitu chema unachomwambia, lakini kadri siku zinavyosonga watajua hayo na mengi yatawakuta na kukumbuka nasaha zako.Unapopanda mbegu ya harage leo usitegemee kuota na kutoa matunda yake siku hiyohiyo. Tenda wema nenda zako.Watakukumbuka daima hata wakianza kujitegemea. Nililea binti wa marehemu mke wa mume wangu sasa ambaye nilimkuta akiwa na miaka miwili.Nilimlea vizuri na alikuwa mtoto mzuri sana.Alipofika miaka 18 amemaliza kidato cha nne na kuanza kidato cha tano alianza mambo ya kikubwa na uongo mwingi akigilibiwa na wenzake, nilipomuonya na kuzingatia masomo alipuuza na kusema kwa wenzake kuwa kwanza si mama yangu kwa nini ananichunga. Matokeo yake form six alipata '0" alilia hadi kujifungia ndani wiki nzima.Nilipata kazi ya ziada kumrejeshea hali yake na kumtia nguvu. Adhabu yake sasa ni kubwa sana kwangu na ni rafiki wa karibu sana na sasa anasoma chuo na amekuwa mzuri na anafanya vizuri. Kwa hiyo dada usivunjike moyo.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-15 12:34:39 [Report Abuse]    
     
  chuo kikuu alifikaje na 0 huyo binti yako wa kambo? hata hivyo ilikuwa rahisi kumlea kwa kuwa alikuwa mdogo sana (miaka 2). Wakubwa kidogo wanakuwa wamekwishajitambua na baadhi wanakuwa wamelelewa vibaya na wazazi wao wa mwanzo.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-15 15:14:17 [Report Abuse]    
     
  Ann wa hapo juu nakujibu, alifaulu vizuri sana form four, alipopata "0" form six aliingia chuo alianza na certificate mwaka mmoja akafanya vizuri na kuendelea na digrii. Hakuna jambo rahisi kwani mama wa kambo ni kambo tu, ndio maana tunamshauri huyo mleta maada kuvumilia,kwani huwezi kumbadilisha mWanadamu kama unavyobadilisha nguo mwilini.Kila jambo linahitaji uvumilivu na hatua kWa hatua. Hata wewe huko ulikotoka na hata Sasa kuna vitabia ulikuwanavyo na na hadi sasa unavyo vingine ambavyo kwa mtu mwingine akikuangalia vinamchukiza.Muhimu ni kuvumilia na kuendelea kulena kwa misingi ya kutokata tamaa.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-16 12:44:28 [Report Abuse]    
     
  sawa dada nimekuelewa. pia nadhani utakuwa nje ya tz maana mfumo wa elimu ya tz mtu mwenye certificate hawezi pata digrii mpaka awe na diploma au advanced certificate.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-20 09:06:26 [Report Abuse]    
     
  Hauko Tanzania na hujui vyuo vya Tanzania wewe.Inelekea unaijua UDSM tu.Mtu akifaulu vizuri certificate anajiunga na Adv Diploma au didrii hapohapo. Nilisoma na wengi kwa mfumo huo na nina ndugu zangu wengi wako vyuo vya Tumaini, Ruaha,Sauti, nk wanaanza na Cerificate na wakifanya vizuri mitihani ya mwisho huendelea hapohapo na digrii au Adv Diploma. Nakushangaa unaposema labda vyuo vya nje ya Tanzania ndivyo vinafanya hivyo, yaani wewe umelemaa na elimu ya Tanzania kuwa ndio iko juu. Nchini Kenya mfumo wa elimu ni mwanafunzai akimaliza form four anaingia chuo kikuu, na huwezi kumlinganisha kijana wa form six wa TZ na kijana wa form four wa Kenya.Wa Kenya anamzidi kabisa huyo wa kwetu licha ya kwamba kamaliza form six.Ndio maana hata ajira WTZ wanazikosa sana hawaezi kushindana na watani zetu.Fumbuka macho hata kilicho nchini mwako hukijui??  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-20 11:05:55 [Report Abuse]    
     
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-20 11:05:55, unaongea kishabiki mno mimi niko nje nimesoma na wakenya wauganda wazambia na mataifa mengine nakuambia lililokweli kabisa darasani watz walikuwa ndiyo wanabeba namba za juu kabisa kisha ndiyo wanakuja hao wengine mtu aliyemaliza tz form six vizuri yaani siyo ile ya kilaza...wakiwa nje wanafanya vizuri sana tofauti na hizo nchi nilizozitaja hapo juu kwanza kuna baadhi ya sirabas wao hawazisomi ambazo ukija huku nje kuchukua Bachelor unazikuta huko tz zinasomwa form six wao wanaanza kusotea tena baadhi ya mambo mengine pia ya form 4 wao wanakuwa hawajasoma kinachokuwa pungufu kwa tz ni ile kiingereza tu ....napo inakuwa kwenye kuongea lakini kwenye kusoma tofauti ni mwenye kufanya vizuri kuliko hizo nchi nilizozitaja tz kinachotakiwa msasa tu wa kiingereza..... lakini katika masomo asikuambie mtu wako fit unless awe na elimu ya kubebwa lakini kama kasoma hasa vizuri form 4 na 6 vizuri, wanafanya vizuri tu...jamani tuacheni huu ushabiki wa kushabikia eti kenya wanaelimu nzuri kuliko tz ni kwakuwa wanaongea kiingereza ni kutokuujua ukweli mimi naona hapa walivyokuwa wanataabika hasa kwenye mwaka wa kwanza wa chuo.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-21 00:21:28 [Report Abuse]    
     
  Bibie mimi mwenyewe niko nje ya nchi.Nimesoma Tanzania vyuo, na bahati nzuri nimesoma Kenya chuo pia. na sasa nimemalizia masomo yangu huku nje. Mimi sijasema Mtaala wa elimu Tanzania ni mbaya kuliko wa Kenya, ila ukweli ni kwamba haumuandai mwanafunzi kujiridhia mwenyewe katika vitendo halisia.Kinachofanyika ni kumkaririsha mwanafunzi na hadi anamaliza ukimwambia hata andika barua ya maombi ya kazi hawezi kwa mpangilio na hawezi hata kuandika CV yake.Nilichoongelea ni namna ambavyo elimu ya wenzetu inavyowanoa katika kupambana na changamoto za uwanja wa elimu na kufit katika kujitatulia mambo.kama unafuatilia habari za Tanzania, mwezi Januari Waziri wa viwanda alitembelea viwanda vya utengenezaji vipuli kule Tanga.Alichoambiwa juu ya ajira ni kwamba wengi wa walioajiriwa ni kutoka Kenya na Uganda kwa sababu wao wakiingizwa kwenye kazi hawangoji kuelekezwa.Watanzania wanajua waliokremishwa pasipo kujua kitu na kitendo chenyewe anachokiimba kwa mdomo.Suala si Kiingereza bali mfumo wetu namna ya kuwajenga wanafunzi wetu kielimu na vitendo. Kwa taarifa yako watanzania wana akili sana, lakini hawana ushirikiano bali wana majungu tu na kuoneana wivu hivyo hata kujifunza kutoka kwa wengine ni vigumu.Niko huku nje kazi kutafutana badala ya kutafuta maisha na kujengana. Ndio maana hata wewe ambaye nahisi ndio mleta maada hapa uko nje na unajeruhiwa na mwanamke mwenzio. NIna Wakenya zaidi ya 800 katika state ninayokaa hawa watu ni wabunifu sana kwa mambo mengi kutokana na misingi waliowekewa kielimu.Licha ya kasoro zao kikabila lakini wanajua sana kusaidiana kwa mengi. Bibie,nakutakia usuluhisho mzuri wa matatizo yanayokusonga katika ndoa yako. Usishindane na mwanaume utaumia sana.Uwe mjanja wa namna ya kumkabili mumeo siyo kuwa mkali itakugharimu sana.Usiige ya huku ughaibuni yana madhara sana.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-21 11:10:39 [Report Abuse]    
     
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-21 11:10:39 ulisoma chuo gani tz??isije ikawa vyuo vyeki vya mzumbe,saut,tumain,cbe,etc...maana tz kuna vyuo vingi vya kuungaunga...unles uwe umesoma udsm maana graduate wa pale bongo zao ziko smart!  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-21 15:48:52 [Report Abuse]    
     
  Mimi nilisoma UD mwaka 1987-91. Kinachoongaliwa si masharti mengi, bali unachozalisha hapo kinakuwa na ubora gani hasa katika soko. Hata hivyo siko kwenye kubishana na wewe maana inawezekana tunatofautiana sana kiwango chetu cha kuelewa, wewe unaelewa hivi na mimi naelewa vile.Bila shaka kila upande una "facts" zake. Ukitaka kuelewa kuelimika kwa waliosoma UD na vyuo hivyo ulivyosema ni vya kuungaunga waweke kwenye soko la ajira na utendaji kazi ndipo utajua nani alielimishwa kwa kufanya kazi na nani alielimishwa kwa kumaliza digrii tu.Nakutakia siku njema. Je kilitokea nini kati ya X mke wa mumeo hadi akatoka hapo na wewe ukaingia hapo?  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-21 17:24:47 [Report Abuse]    
     
  Kuna watu bado wanaamini kuwa chuo ni UD tu?? Mbona tunabanana kwenye interviews???? Na chama ni CCM tu au???? Lol.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-24 14:22:14 [Report Abuse]    
     
  Tena kuna rafiki yangu kaunga unga kamaliza degree ya kwanza Tumaini na sasa anafanya MBA UD bado utasema chuo ni UD tu; kwa nini wanawapa admission za masters watu wa vyuo vingine mnavyoona vya chini. Endeleeni kujiaminisha kuwa nyie ni bora zaidi; mkijashtuka mmetupwa kuleee.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-24 14:31:22 [Report Abuse]    
     
  Mwambieni huyo bibie anayesema UD mlimani ndio eti wako smart na amevitaja vyuo vingine kuwa ni vya kuungaunga.Mbona yeye ameungaunga ndoa maana huyo mwanaume alikuwa na mke wa kwanza ambaye ndiye kazaa hao watoto anaolialia nao kuwa hawaambiliki.Kama ana dharau kihivyo na ubishi mwingi huo atakubaliana vipi na mumewe?Nimemshtukia kumbe matatizo ni yake mwenyewe kwa sababu ni mbishi na dharau. Mheshimu mumeo matatizo yako yataisha.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-25 14:10:15 [Report Abuse]    
     
  nyie wote mlioongea ambao hamjasoma UD ni vilaza...pure vilaza...msijidanganye wala kujifariji sijui tumain,mzumbe,etc hivyo vyuo vyote wanaenda second class students...first class & smart students wanakwenda UDSM then waliobakia ndo huko kwingine....kulinganisha udsm na mzumbe/tumaini/etc ni sawa na kulinganisha havard univrsty na wichita univ kwa marekani...no matter what happens to them aftwards;students who go to UDSM are cream of the Nation!!  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-26 02:13:47 [Report Abuse]    
     
  Wewe Ann wa hapo juu,Umeamka bila kuomba na kumshukuru Mungu ndio maana ukakimbilia kuandika matusi hapa kuwa wenzio ni vilaza. Mbona mimi mdogo wangu alipata division 11 anasoma hapo?mbona mtoto wa kaka yangu mwaka jana alipata dv 11 anasoma hapo Ecnomics kama kweli wanaochaguliwa hapo ni first class?Mbona kaka yangu alisoma Tumaini Univerosty Iringa first degree sasa hivi yupo UDSM kufanya masters ya MBA?Inakuwaje wamchukue mtu wa vyuo vya chini kusoma katika chuo cha juu?Bila shaka wewe unazungumzia juu ya ukongwe wa UDSM na kulinganisha na upya wa vyuo vya sasa.Umenichekesha sana wewe, na hiyo migomo yote ya wanafunzi UD wanasoma saa ngapi mpaka wamalize hata mitaala wawapite ubora wanafunzi wa vyuo vyote ulivyovitaja kuwa havina ubora?Ningekuwa dunia nyingine ambayo siwajui waliosoma UD ungenidanganya sana wewe? Unadhani kipimo cha kufaulu kidato cha sita kupata DV 1 ni kipimo cha ubora wa mwanafunzi aanzapo chuo hadi kumaliza?Kama ingekuwa hivyo mbona wana-supple, na mbona wanapata madaraja hadi ya sifuri kama chuo kinatoa watu waliofaulu sana hizo feria zinatoka wapi? Je, una habari kwamba watu wengi wenye nafasi nzuri huwa wanawaondoa watoto wao kusoma UD wanawapeleka SAUTI,TUMAINI na kwengineko?Wanaosoma UD ni watoto wa maskini miaka hii ambao wazazi wao hawawezi kuwalipia ada ya vyuo vya binafsi. Ngoja nikuache maana ukweli upo bayana ya nini kubishana wakati soko liko nje tu wote tunawaona wakipwaya??  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-26 11:47:15 [Report Abuse]    
     
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-26 11:47:15 unakielewa unachoongea ama?.hv unajua ubora wa chuo unapimwaje?chuo kinapimwa kulingana na no ya professors&doctors na idadi ya scientific researchz zinazofanywa...hivyo vyuo vya kata unavyovisema malecturer wao wengi ni vijana wenye masters tu ambao kwa chuo kama UDSM hao ni tutorial assistants...unakuta kijana amesoma kuanzia mwaka wa kwanza hadi anamaliza kwenye hivyo vyuo hawajawahi kufundishwa na prof..hao watu unaosema cjui wanauwezo wanapeleka watoto wao tumaini,saut ni sbbu watoto wao wenyewe ni vilaza..matajiri wengi tz watoto wao ni vilaza!..nasema haya kwa evidence ya vijana hao wa vyuo other than UDSM wanavyokuja kufanya practical training maofisini unakuta hamna kitu mpaka unajiuliza wako chuo au?  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-27 01:17:10 [Report Abuse]    
     
  Ann hapo juu nakuunga mkono. Nakumbuka nikisoma UD mwaka 2004 class la comp scnce tukiwa wanafunzi 40 wote tulikuwa ni division one kali mpaka nikawa naogopa naweza kuwa wa mwisho kwenye pepaz haha!chezeyaaa udsm students. Jenne  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-27 01:44:49 [Report Abuse]    
     
  Pole Kissa kwa yaliokukuta.Inauma sana usiombe yakukute.Napia hongera kw a kuwa mama mwema.Mi ushauri wangu wala usijipe shida eti kumzuia asiende kumwona,huyo tayari ni mwanae,hata akienda utajua?Kumbuka kuwa hata huyo mwanamke umekuja jua tayari mtoto ana mwaka. Hilo lililokukuta hata mimi lilishanitokea miaka 2,iliyopita.Nilileta suala langu hy,nikapewa ushauri ambao ulinsaidia sana.Mi bahati nzuri sikuwahi na wala sijawahi hata siku moja kujihangaisha kumpigia simu huyo mwanamke.Nilidili tu na mume wangu.Sielewi mwenzangu una shughuli gani ya kukuingizia kipato lakin mimi ni mwajiriwa,kwa hiyo nilichokifanya nikaongeza ubusy wa kutafuta pesa,outing na rafiki zangu kwenda kujipa raha,mwisho wa siku nikanunua na kiwanja nimejenga self contained house ya 3rooms.Nikasema hii biashara ya huyu kanunua cementi mi nimeleta lori la mchanga mwisho wa siku mali zinakuwa za watu lukuki siwezi.Na ukichukulia mama wa huyo mtoto ye hana kazi yoyote kwa hiyo,kila kitu ni mume wangu.Sasa hivi mwanaume kageuka ye ndo ananizulia nina mwanaume,kisa"mbona haoni nagusa simu yake"Ushauri anaonipa eti jua kuwa watoto wetu bado wadogo,usije ukawa unahangaika na wanaume huko nje.Nachomjibu ni kuwa sijihangaishi na simu ya mtu nisijekufa kwa pressure bure nikaacha wanangu.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-27 08:46:41 [Report Abuse]    
     
  Kijana hujajibu maswali niliyokuuliza maana mimi nilikujibu kulingana na hoja yako ya kwamba wanaoingia UD ni first class tu ndipo nikakupa mifano halisia. Pia ungejua unaongea na nani nadhani ungenyamza tu na huko kujisifu kwako na kuwaita wenzako vilaza. Kwa ufahamu tu ubora wa chuo haupimwi na kuwa na maprofesa wengi katika chuo. Ni muhimu ujue kuwa uprofessa wa TZ ni wa kupeana tu. Nimefundishwa hapo hapo UD na Maprofessa ambao huwezi hata jua huo uprofesa waliupataje?Ni nafuu ukafundishwa na mwenye masters utaelewa na kujengeka na unachofundishwa. Kuwa na vitendea kazi vingi si ubora wa ufanisi wa kazi. Unaweza kuwa na maprofessa wababaishaji.Nilipokuwa UD mara zote hao wanaojiita maprofessa walishindwa kumaliza hata mtaala.Kupimwa kwa chuo kuwa na wasomi wa ngazi ya Professors and doctors and reseacher wise kama ndio kiegezo cha ubora wa chuo nakubaliana na wewe na hiyo ndio sera ya uanzishaji wa vyuo vikuu. Lakini bado ujue kuwa unaweza kulundika watu wa namna hiyo ukidhani umeweka watu wa maana kumbe umeweka ubabaishaji. Ni sawa na usemi ule wa "Mtu kapata kazi lakini kazi haijapata mtu" Najiaminisha kusema mengi kwa sababu nimepitia hapo UD na kwenda mbele zaidi. Kwa hiyo huwezi kunidanganya na hizo Dv 1 za utapeli na ufisadi mtupu.Mtu anaweza kutibiwa vizuri kwenye zahanati kuliko hospitali ya Taifa Mhimbili. Hata hivyo sitaki kubishana nawe maana mimi nina ushahidi wa kutosha na kila kilicho ndani ya UD. Kumbuka kwenye miti mingi hakuna wajenzi. Maprofessor wa mlimani wapo tu kung'ang'aniana vijisenti kwenye idara zao na kupigana vikumbo na chuki kemkem.Nenda pale ukaulize.Ndio maana migomo ni sehemu ya elimu ya UD. pamoja na hayo nakiheshimu sana chuo kikuu cha Dar kama msomi aliyepita hapo,lakini sina sababu ya kuona vyuo vingine viko chini, kwani ninachoangalia ni ubora wa uzalishaji wake na siyo uingizaji wa wanafunzi bora.Kuna vijana wanafaulu shule za kata kuingia high school,na wakifika huko hufanya vizuri kuliko waliotoka hata shule zinazoitwa bora.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-27 11:29:27 [Report Abuse]    
     
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-27 08:46:41 hongera sana.Salua.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-28 01:02:40 [Report Abuse]    
     
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-27 11:29:27 naona bado unaongea hueleweki. Umesema umepitia UD?kweli?au wewe ni mmoja wa wale mlioingia kwa equivalent qualification na si direct entry?au wewe ni mmoja wa wale mliongizwa kwa upendeleo maalum wa gender (na huu utaratibu ndio unaanza kuzalisha graduate wa UD wasio na weledi wa fikra&kuchanganua mambo)..ulipata div gani high school na points ngapi?UD ulisoma course gani?..hoja yako ya kusema cjui maprof wababaishaji unailewa kweli?kwa taarifa yako 98%ya profs wa UDSM wamepata uprof wao vyuo best vya nje ya tz!.migomo ya wanafunzi wa UD ni kutokana na bongo zao kuchemka zaidi so si watu wa kukubalikubali tu mambo bila strong arguments!.unasema chuo kiangalie cjui uzalishaji na si ubora wa wanafunzi wanaoingia?are you serious?unadhani Havard au Oxford univ wanapokea tu wanafunzi ovyo-ovyo?you nid to be cream&highly brainy kujiunga nao so applies to UDSM.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-28 03:26:49 [Report Abuse]    
     
  Nadhani anny unaesema maprof wa UD ulikuwa huwaelewi nadhani sababu labda uwezo wako wa uelewa ulikuwa mdogo sana then ukajikuta unafundishwa na walimu mwenye uwezo mkubwa sana. Nakumbuka wakati nasoma chuo kimoja kulikuwa na wanafunzi uelewa wao ulikuwa wa chini sana so maprof wakilecture (sio kuandika notisi ubaoni) wale wanafunzi wakawa hawaoni kitu mwisho wa siku wakawa wanategemea discussion kueleweshwa na wenzao.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-28 03:57:03 [Report Abuse]    
     
  Hao watoto bado ni wadogo. Lazma waimizwe na waambiwe, ndio maana ya kulea, soma saikologia ya watoto wa umri uwo. Hata wakawa na mika 20 lazma mtoto ambiwe na afundishwe na aimizwe. Ila kwa vile watoto sio wako, picha inakuwa ingine. Waswaili walisema mavi ya mtoto wa mwenzio yananuka. Ila mavi ya mtoto wako hata na mkono unazoa. swali kwanini hawaishi kwa mama yao? Huyo mumeo anaku use wewe kama mlezi nazani na vile vile hakueshim na wala hakupendi. Mshenzi tu. Malaya. Hachana nae, azoe mavi ya watoto wake mwenyewe. kama amekutoa afrika, kwa vile umezaa nae haki ya kuishi uko unayo, serikali haiwezi kukurudisha tz. Huyo bwana atakuletea mtoto mwengine na mwengine na hata ukifanya nini atakuambia hivo hivo uwapendi kwa vile si wako. Maisha mema.  
  Reply by: KEMI, Date: 2012-06-29 05:15:17 [Report Abuse]    
     
  Ahsante da Salua,unajua hawa watu si tunayotulia huwa wanatuona kama wajinga fulani,kumbe mtu unafikiria mengi na karne hii magonjwa kibao.Lakin inabid kufunga mkanda maana ukiwafuatilia sana utakufa uache watoto, naye baada ya siku tatu anaoa mwanamke mwingine.  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-06-29 08:14:12 [Report Abuse]    
     
  ^&($Cheers for the info. Greatly appreciated. [url=http://www.iamsport.org/pg/blog/sikesa9057/read/13350096/and-offering-the18-wheeler-an-excellent-meaner-glimpse]Ugg Boots Outlet[/url] Ugg Boots Outlet  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-12-11 13:46:53 [Report Abuse]    
     
  ^&($Curious to determine what all you intellectuals need to say about this?-?-. Uggs Outlet  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-12-11 14:07:12 [Report Abuse]    
     
  *()&It really is good to possess the capacity to examine a great high quality article with practical specifics on topics that plenty are interested on. The stage that the information indicated are all first hand on reside experiences even guide a lot more. Proceed performing what you do as we really like readi?- Michael Kors Outlet  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-12-14 06:14:41 [Report Abuse]    
     
  *()&One of the best sites for relevant facts on this niche !?! Coach Outlet Online  
  Reply by: Anonymous , Date: 2012-12-17 00:09:10 [Report Abuse]    
Submit your comment here...!
  Topic nahitaji mawazo yenu
  Reply
  Email Login/Register to use your username! (Click here)
   
  Enter Code
   
     
<<Back to Topics<< >> Reply to this message>><<EMAIL ME FOR NEW POST <<
womens pants, wedding dresses, wedding pictures, women shoes, wedding accessories, women nails, women hair, women message women send off, good wedding shoes and hotels
Any use of materials or photographs from HarusiYangu is strictly prohibited
© 2007. All Rights Reserved Designed and maintained by Bomba Designs